Waziri mkuu Kassim Moajaliwa amekutana
na mabalozi wa Tanzania wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi
mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki kati ya
nchi wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi,ikiwa ni
pamoja na kueleza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo nchini.
Mabalozi wa Tanzania walioteuliwa hivi
karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kuwakilisha
Tanzania nnje ya Nchi,wamefika ofisi ya waziri mkuu mjini Dodoma kwa
lengo la kumuaga na kwenda kuanza majumukumu yao katika nchi
walizopangiwa.
Waziri mkuu amewaleeza mabalozi hao kuwa
Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji Na jukumu lao la kwanza la
Mabalozi hao ni kuvitangaza vivutio vilivyopo ili kuleta wawekezaji
wengi TANZANIA .
Suala la ushirikishwaji sekta binafsi pia waziri mkuu amesema Tanzania imelipa kipaumbele
Waziri Mkuu alizungumzia sula la
watanzania waishio nje ya nchi , aliwataka Mabalozi kuwakutanisha na
kufanya nao mikutano mara kwa mara ilikujua kama wanamatatizo
yanayoyapata katika nchi wanazoishi ilikuangalia jinsi gani wanaweza
kusaidiwa,
Mabalozi hawa wanaenda kuiwakilisha
Tanzania katika nchi za QATAR,UBELIGIJI,AFRIKA
KUSINI,UJERUMANI,COMORO,ALGERIA,INDIA NA ,SUDAN.
0 comments: