Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Septemba 24, 2017 limetoa
ufafanuzi na uthibitisho wa risiti ya malipo ya fedha za wabunge milioni
43 kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu ambazo zilichangwa na wabunge
na kulipwa hospitali ya Nairobi.
Bunge limelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa
hospitali ya Nairobi mbaka jana ilisema haijapokea fedha hizo kutoka kwa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Ofisi ya Bunge inapenda kusisitiza kuwa fedha zilizochangwa na Wabunge
kiasi cha Tsh. Milioni 43 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mheshimiwa
Tundu Lissu tayari zimetumwa katika Akaunti ya Hospitali ya Nairobi
anakopatiwa matibabu. Fedha hizo zimetumwa kupitia Benki kuu ya Tanzania
(BOT) ambapo kwa mujibu wa viwango vya kubadilishia fedha vya BOT kwa
siku hiyo ilikuwa ni sawa na Shilingi ya Kenya 1,977,120.58." ilisema
taarifa ya Bunge
Taarifa hiyo ya Bunge iliendelea kusisitiza kuwa walituma fedha hizo Septemba 20, 2017
"Kiasi hicho cha Fedha kilitumwa siku ya tarehe 20 Septemba, 2017 kwenda
Benki ya Barclays, Tawi la Hurlringham, Akaunti Namba 0451155318 yenye
jina la Kenya Hospital Association"
Septemba 22, 2017 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alisema kuwa mbaka
siku hiyo anatoa taarifa mbalimbali kuhusu Tundu Lissu fedha ambazo
wabunge walikuwa wamechanga kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu
zilikuwa hazijafika Hospitali Nairobi Kenya, lakini siku moja baadaye
Bunge lilitoa taarifa na kusema walikuwa wameshatuma fedha hizo toka
Septemba 20 mwaka huu, baadaye zikawepo taarifa kutoka hospitali ya
Nairobi kuwa bado hawajapata fedha hizo kutoka Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
0 comments: