Baada ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kusikika wakidai vyombo vya usalama kutoka nje ya nchi vije kufanya
uchunguzi wa shambulio la MbungeTundu Lissu, Msemaji mkuu wa Serikali
Dkt. Hassan Abbaas amefunguka na kuhoji watu wangapi wamekufa na wazungu
hawakuja.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt. Abbas amehoji kwa kuandika "Waje
wazungu? Wamekufa watu wangapi Kibiti hatukuita wazungu?Lakini hatujui
pia hata hao wazungu kwao makosa ya jinai pia yamewazidi nguvu?
Hata hivyo Dkt Abbas ameongeza kwamba tabia ya kutuhumiana kunapotokea
kosa la jinai ambalo limetendwa kwa mtu yoyote au mwanasiasa siyo vizuri
kwani kufanya hivyo kunakufanya uwe mshukiwa namba moja wa tukio.
Ameongeza kwamba kwamba ni "busara vyombo vya dola vikaachwa vifanye kazi yake kwanza na siyo kutuhumu".
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kupitia viongozi wake wamekuwa
wakitaka serikali iruhusu vyombo vya kimataifa waje nchini kufanya
uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu aliyepigwa risasi na waru
wasiojulikana Septemba 7 akiwa nje ya nyumba yake Area D' Dodoma
alipokuwa akitokea bungeni mchana.
0 comments: