Waziri
Ummy Mwalimu amejibu tuhumu zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya
serikali baada ya kutaka kuombwa kugharamia matibabu ya Lissu, na kusema
kwamba serikali imelazimika kufanya hivyo kwa sababu mgonjwa alijitoa
kwenye utaratibu wa serikali.
Ummy
Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, ametoa maelezo hayo leo kwenye ukurasa wake wa twitter, na
kusema kwamba serikali isingeweza kuingilia kati bila kuombwa na familia
ya Tundu Lissu, kwani mgonjwa alishatolewa kwenye utaratibu wa serikali
kwa kupelekwa Nairobi, na hiyo sio mara ya kwanza kwa serikali kufanya
hivyo.
"Mgonjwa
alitolewa kwenye utaratibu wa serikali alipopelekwa Nairobi, sasa
gharama/tiba zaid yahitajika, serikali inaingiaje bila ridhaa ya
familia? Na hii sio mara ya 1 kutokea. Mzee wetu S.Sitta (RIP),
alikwenda matibabu London kwa utaratibu binafsi kisha alileta maombi
serikali ishiriki", ameandika Ummy Mwalimu.
Waziri
Ummy Mwalimu ameendelea kwa kuandika akisema kwamba mgonjwa ni Mbunge
anayehitaji matibabu zaidi, lakini kwa kuwa sasa hivi yupo nje ya
utaratibu wa serikali, ili serikali iweze kushiriki ni lazima yawepo
maombi ya kufanya hivyo.
Hapo
juzi serikali ilitoa tamko ikisema kwamba watakubali kusimamia matibabu
ya Tundu Lissu popote duniani iwapo familia yake itaomba kufanya hivyo,
na sio vinginevyo, kitendo ambacho kimeibua sintofahamu nyingi kwa
baadhi ya wananchi wakiilaumu serikali kwa kutojali matatizo ya Tundu
Lissu.
Mgonjwa alitolewa kwenye utaratibu
wa Serikali alipopelekwa NRB. Sasa Gharama/Tiba zaid yahitajika.Serikali
inaingiaje bila RidhaaYafamilia?
0 comments: