Humphrey
Polepole amefunguka na kusema Rais Magufuli hakuwahi kuwa na nafasi ya
uongozi ndani ya Chama hicho na kudai ndiye alikuwa mtu sahihi 2015
kwani alipoingia ndani ya chama na serikali ameweza kuona matatizo
ambayo wengine hawakuweza kuyaona.
Polepole
amesema kuwa kwa jinsi ambavyo chama hicho kilivyokuwa kipindi cha
nyuma kilihitaji mtu ambaye hayupo ndani ya mfumo wake ili aweze kuona
mapungufu mbalimbali ndani ya chama na serikali.
"Ndugu
Magufuli kama Mwenyekiti ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa ni
kiongozi wa kawaida na duniani kote unaposoma elimu ya mageuzi huwa
inataka upate mtu ambaye ni wa kawaida labda huenda asiyetoka katika
eneo ambalo linafanyiwa mageuzi ili aweze kuwa na jicho la nje, kwa
sababu gani wewe unayekaa ndani unaona kama mambo yako sawa hivi, sasa
ndugu Magufuli ndani ya CCM hajawahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu,
hajawahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, hajawahi kuwa Mjumbe wa Sekretarieti
sasa CCM ilipotafakari ni nani atakayeweza kufanya mageuzi makubwa
ndani ya chama hivyo hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya John Pombe
Magufuli" alisema Polepole
Aidha
Polepole amesema kuwa Rais Magufuli alipoingia serikalini na ndani ya
Chama Cha Mapinduzi hakuona haya kusema madudu na uozo uliopo ndani yake
"Magufuli
hajaona haya kusema kwanini dhahabu inaondoka mnaitazama, Kwanini hii
Almasi inakwenda na kwanini tunashindwa kuichakata hapa, kwanini
bandarini mnaruhusu mizigo inaingia bila kulipa kodi, na nyinyi CCM
kwanini mali zenu zinahodhiwa na watu na fedha haziji kwenye chama, hii
yote ni kwa sababu anajicho la nje ambaye anaona tofauti na nyinyi
mliopo ndani ya ambao mshazoe" alisema Polepole
Mbali
na hilo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
amesema kuwa anapomsikia Rais Magufuli akisema kuwa nafasi ya Urais ni
kazi ngumu anamuelewa kweli na kusema kuwa yeye anajua uongozi si kazi
ya furaha bali ni mzigo mkubwa.
0 comments: