NI PAVEA NA NAMANJI HASHIMU
Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amewasilisha vielelezo vingine
katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili
kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi ya viongozi wa Serikali wanaodaiwa
kuwanunua madiwani wa Chadema waliohamia CCM.
Nassari aliwasili katika ofisi hizo jana saa 7:57 mchana na kutoka saa 11:33 jioni.
Wakati
Nassari akiendelea na mahojiano hayo, maofisa wa Takukuru waliwafukuza
waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakisubiri kufanya
mahojiano na mbunge huyo.
Hata
alipotoka alikuwa amesindikizwa na maofisa hao waliokuwa wakiwazuia
waandishi ambao waliamua kumsubiri nje ya lango la ofisi hizo wasifanye
mahojiano.
Mmoja wa maofisa hao alimsindikiza mbunge huyo hadi alipohakikisha ameingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo.
Nassari aliwataka waandishi wamfuate katika eneo jingine kwa ajili ya mahojiano.
Akieleza
sababu za mahojiano yake kuchukua muda mrefu, Nassari alisema hilo
limesababishwa na wingi na uzito wa vielelezo alivyokuwa navyo.
“Nimewasilisha vielelezo na nimefungua jalada, nikatoa maelezo yangu mengine nimewaachia wao waendelee na uchunguzi.
“Ushahidi
nilionao ni mkubwa mno umehusisha viongozi wengi, nami nimetoa kila
nilichonacho na kuna nyaraka nyingine zipo Arusha zikifika kwa wakati
muafaka nitaziwasilisha,” alisema.
0 comments: