Mtandao wa Elimu (TEN/MET) kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania
wawakutanisha walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania ili kutafuta mbinu za
kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma au kukwamisha jitihada
zao za kutoa elimu bora nchini.
Meneja Miradi wa Mtandao huo, Mwalimu Alistidia Kamugisha (wa kwanza
kulia) Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kongamano hilo.
Akizungumza wakati wa utambulisho na lengo la kongamano hilo maalumu
katika siku ya Mwalimu duniani, Afisa miradi ya mtandao huo Mwl.
Alestidia Kamgisha alisema walimu wanachangamoto nyingi ambazo
zisipotatuliwa zitaendelea kushusha ubora wa elimu kutokana na
kuporomoka kwa hali ya mwalimu kufundisha.
“Kukutana kwao kwa pamoja kutasaidia kila mmoja kusikia changamoto na
mafanikio ya mwalimu mwenzake kutoka mkoa mwingine lakini pia kujifunza
kwa walimu wengine waliofanikiwa wakiwa ndani ya changamoto hizo”,
alisema Kamugisha.
Pia Afisa Miradi huyo wa mtandao wa elimu Tanzania aliongeza kuwa
mawazo ya pamoja kutoka kwa wadau hao yatasaidia katika kubuni mbinu za
pamoja kama wadau ili kusaidia kutatua chaangamoto hizo na kurudisha
nguvu ya mwalimu katika kufundisha na kufaulisha.
Aidha akieleza hali ya shule yake mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Nyandira mwalimu Atulinda Musebura alisema kuwa shule yake inawalimu
watano tu lakini inazaidi ya wanafunzi 1000 idadi ambayo ni kubwa sana
kwenye uwiano kati ya mwalimu mmoja na mwanafunzi.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu Atulinda Musebura.
“Hali hii inatulazimu kufundisha kwakuelekeza nguvu kwa darasa la saba
ili kuwawezesha wanafunzi hao kufaulu mitihani yao ya mwisho na
wanapoondoka nguvu zetu tunazielekeza kwa darasa la nne ambao nao
wanakuwa na mtihani wa Taifa,
Hali hiyo inawanyima wanafunzi wengine kwenye nyakati Fulani kukosa
masomo na hata kuwatesa walimu hao kwa kufanya kazi kupita uwezo wao na
mwalimu anapopata dharura hali huwa mbaya zaidi kwani walimu hao kila
mmoja anavipindi zaidi ya 67 kwa wiki badala ya 40”,alisema Musebura.
Kwa upande wake muwezeshaji kwenye kongamano hilo bwana Zelote
Loilang’akaki alisema mkakati wa serikali kutoa elimu bure umesaidia
kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi mashuleni lakini swala la
ongezeko la walimu halikuzingatiwa hivyo kuwafanya walimu kuzidiwa na
mzigo wa kazi ya ufundishaji.
Mwezeshaji wa kongamano hilo Bwana Zelote Loilang’akaki akizungumza na washirki hao
“Changamoto ya upungufu wa walimu umekuwa mkubwa kwa shule za msingi
wakati wa idadi ya walimu wa Sayansi ikibaki kuwa ndogo kwenye shule za
secondary kwamfano kuna upungufu wa walimu wa Sayansi 64 sekondari
wakati msingi kunaupungufu wa walimu 614 kwa mujibu wa ripoti za
TEN/MENT kwa wilaya ya Mvomero pekee”, alisema Loilang’akaki.
Pia alibainisha kuwa kwa mujibu wa serikali idadi ya walimu imeongezeka
kufika 165,856 mwaka 2010 hadi 2011 hadi kufika 190,957 mwaka 2014 hadi
2015.
Taarifa za chama cha walimu Tanzania (CWT) zinaonyesha nchi inaupungufu
wa walimu 100,000 kwa shule za msingi 500,000 shule za sekondari ambapo
walimu wa Sayansi 30,000 na sanaa 20,000 huku taarifa za elimu ya msingi
(BEST 2016) zinaonyesha upungufu ni walimu 7291 wa hesabu 5118 Biology
5375 kemia 6873 walimu wa fizikia.
Siku ya walimu duniania mwaka 2017 imebeba ujumbe usemao “mwalimu
anastahili mazingira bora na huru ya kufundishia: kodi anayolipa itumike
kwaajili ya kumjengea uwezo na kuboresha mazingira yake”.
Bwana Prosper Lubuva Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo (CWT)
akiwasilisha mada juu ya mapendekezo ya Shirika la kazi duniani na ILO
na UNESCO kuhusu hali ya walimu ya mwaka 1966.
Mwalimu akiwa amefungwa kitambaa na kuagizwa kitu ukumbini hapo ikiwa
ishara ya kuona changamoto na vikwazo anavyokutana navyo Mwalimu kwenye
kufikia malengo yake ya kufundisha na kufaulisha.
Wadau hao wakifuatilia mada ya mapendekezo ya hali ya mwalimu duniani.
Baadhi ya wadau hao wa Elimu wakifuatilia kongamano hilo.
0 comments: