Mugabe Akubali Yaishe.....Ang'oka Rasmi

Shangwe zimelipuka jijini Harare nchini Zimbabwe baada ya Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe kuakubali kujiuzulu jana Jumanne jioni.

Shangwe hizo zililipuka baada ya nchi hiyo kuwa katika presha kwa siku kadhaa baada ya wanajeshi kumweka kizuizini Rais Mugabe huku wakifanya utaratibu wa kumtaka aondoke madarakani.

Mugabe (93) amekuwa kiongozi wa nchi hiyo kwa miaka 37 na kuanzia wiki iliyopita kumekuwa na mchakato wa kutaka kumwondoa hadi leo alipoamua kuliandikia Bunge barua ya kujiuzulu.

==>Hii ni barua ya Mugabe Kujiuzulu

Advert
Share on Google Plus

0 comments: