Rais Magufuli Amteua Rutageruka Kuwa Mkurugenzi Mkuu TANTRADE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Edwin Novath Rutageruka kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa  tarehe 21 Novemba, 2017 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Edwin Novath Rutageruka umeanza tarehe 11 Novemba, 2017.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Edwin Novath Rutageruka alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

21 Novemba, 2017
Share on Google Plus

0 comments: