Mamlaka
ya udhibiti wa mawasiliano nchini (TCRA) imekitoza kituo cha redio cha
Clouds FM faini ya shilingi milioni 12 ikiwa ni pamoja na kupewa onyo
kali kwa sababu ya kukiuka maudhu na kanuni za utangazaji kupitia
vipindi vya Jahazi na XXL.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar, Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema Clouds FM imetozwa shilingi
milino tano kwa kosa la kukiuka misingi na maudhui ya utangazaji kupitia
kipindi cha Jahazi kwenye kipengele cha Mastori ya Town, shilingi
milioni tano kupitia kipindi cha Jahazi kipengele cha Najua Wajua na
shilingi milioni mbili kupitia kipindi cha XXL.
“Hata
hivyo, tunaitaka Clouds Media Group kuwaomba radhi wasikilizaji wa
vipindi hivyo kwa siklu tatu mfululizo na pia tunautaka uongozi wa
Clouds Media Group kuwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji
wanaokiuka maadili, miiko na kanuni za utangazaji,” alisema Mapunda.
0 comments: