SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA KWA WATEJA WALIOUNGWA KATIKA GRIDI YA TAIFA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa mnamo majira ya Saa moja na dakika mbili asubuhi imetokea hitilafu katika Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha Mikoa yote iliyo unganishwa katika Gridi kukosa umeme.
Jitihada zinaendelea kurejesha umeme kwa haraka na tutaendelea kutoa taarifa zaidi.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
30/11/2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: