SHIRIKA LA UMEME TANESCO LA TOA TAARIFA KWA UMMA

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA KWA WATEJA WALIOUNGWA KATIKA GRIDI YA TAIFA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa mnamo majira ya Saa moja na dakika mbili asubuhi imetokea hitilafu katika Gridi ya Taifa na hivyo kusababisha Mikoa yote iliyo unganishwa katika Gridi  kukosa umeme.

Jitihada zinaendelea kurejesha umeme kwa haraka na tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd /twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

30/11/2017

0 comments:

Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge kuhusu Wabunge wa CUF wanaodai kurudishiwa ubunge wao


Ofisi ya Bunge imesema hakuna sehemu katika uamuzi wa Mahakama Kuu dhidi ya wabunge wanane wa viti maalumu CUF waliofukuzwa uanachama na chama hicho inayosema  wanatakiwa kurudishwa bungeni.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ulitolewa Novemba 10,2017 katika Kanda ya Dar es Salaam umeizuia CUF kujadili na kuwafukuza uanachama wabunge hao na madiwani wawili wa viti maalumu.

Hata hivyo, Mahakama ilitoa uamuzi huo huku tayari chama hicho kikiwa kimeshawavua uanachama na baadaye kupoteza nafasi zao za ubunge.

Wabunge hao ni Miza Bakari Haji, Saverina Mwijage, Salma Mwasa, Raisa Mussa, Riziki Mngwali, Hadija Salum Al-Qassmy, Saumu Sakala na  Halima Mohamed.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 30,2017, Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema shauri lililofunguliwa ni kupinga uamuzi wa CUF kuwafukuza uanachama na kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama bado uamuzi wa mwisho haujatolewa.

"Uamuzi uliotolewa na Mahakama ni wa awali kuhusu pingamizi na uliwalenga walalamikiwa ambao ni baraza la wadhamini wa CUF na uongozi wake ambao uliamuru walalamikiwa wasitishe utekelezaji wa uamuzi wa kuwafukuza uanachama na vilevile, kutojadili suala lolote kuhusu uanachama  wa walalamikaji hao hadi Mahakama itakapokamilisha shauri la msingi," amesema.

Amesema ifahamike vyema kuwa hakuna sehemu yoyote katika uamuzi huo wa Mahakama inapoelekezwa wabunge hao wanatakiwa kurudishiwa ubunge.

Kagaigai amesema kumekuwapo tafsiri isiyo sahihi ya uamuzi huo wa Mahakama inayotolewa na baadhi ya watu na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya jamii kusambaza taarifa potofu kuwa wabunge hao wamerejeshwa bungeni kwa uamuzi huo wa Mahakama  baada ya kurejeshewa uanachama wa CUF.

Amesema wabunge hao waliiandikia ofisi ya Bunge barua wakiomba kufahamishwa utaratibu utakaotumika kuwarejesha bungeni.

"Tunapenda umma uelewe kwamba, nafasi za ubunge zilizoachwa wazi baada wabunge husika kufukuzwa uanachama zilijazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria na wabunge waliopatikana kujaza nafasi hizo wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo," amesema.

0 comments:

Mbunge wa CUF Ashinda Pingamizi la Serikali Mahakamani

Mbunge wa Malindi (CUF), Ally Saleh ameruka kihunzi cha Serikali mahakamani, baada ya kushinda pingamizi la awali lililowekwa na Serikali katika kesi ya kuhoji uhalali wa wajumbe wapya wa bodi ya wadhamini wa chama hicho.

Saleh ambaye pia ni mwanasheria amefungua kesi Mahakama Kuu akihoji uhalali wa wajumbe wapya wa bodi waliosajiliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

CUF imegawanyika pande mbili; inayomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na inayomuunga  Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ambaye ndiye aliunda bodi inayopingwa.

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Ofisa Mtendaji wa Rita, anayewakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupitia jopo la mawakili wa Serikali linaloongozwa na Gabriel Malata.

Wengine ni bodi ya wadhamini (mpya) ya CUF, mwenyekiti wa bodi hiyo, Peter Malebo, wanaowakilishwa na wakili Majura Magafu na wajumbe wapya wa  bodi hiyo wanaowakilishwa na wakili Mashaka Ngole.

Wadaiwa wengine ni wajumbe wa bodi waliomaliza muda wao na ambao wengine walipendekezwa tena na upande wa Maalim Seif ambao hata hivyo hawakuidhinishwa na Rita, wanaowakilishwa na mawakili Juma Nassoro, Daimu Halfan na Hashim Mziray.

Serikali kwa niaba ya mdaiwa wa kwanza (Mtendaji wa Rita), iliweka pingamizi la awali ikiiomba Mahakama iitupilie mbali kesi, ikitoa hoja kuwa imefunguliwa kabla ya wakati bila kufuata utaratibu wa kuishtaki Serikali na kwamba mdai amemshtaki mtu asiyestahili.

Saleh anayewakilishwa na mawakili Mpale Mpoki na Fatma Karume, ameshinda pingamizi hilo katika uamuzi uliotolewa na Jaji Wilfred Dyansobera alioutoa jana Jumatano, Novemba 29,2017.

Jaji Dyansobera ametupilia mbali pingamizi hilo la Serikali baada ya kuridhika kuwa hoja za pingamizi hilo hazikuwa na mashiko.

Wakati wa usikilizwaji wa pingamizi hilo, wakili Malata alidai mdai amemshtaki mtu asiye sahihi; akidai Rita ni wakala ndani ya ofisi ya Kabidhi Wasihi Mkuu ambaye ndiye aliyestahili kushtakiwa na si mtendaji wa Rita.

Pia, alidai kesi ilifunguliwa kabla ya wakati kwa kuwa ilifunguliwa kabla ya kutoa taarifa ya kusudio kwa Serikali ya siku 90, kama inavyoelekezwa katika sheria ya mashauri dhidi ya Serikali.

Wakili Mpoki alipinga hoja hizo akidai mtu waliyemshtaki ni sahihi na kwamba, kwa aina ya kesi hiyo hapakuwa na haja ya kutoa taarifa ya siku 90 kwa Serikali kwa kuwa hawaishtaki Serikali.

Jaji Dyansobera katika uamuzi wake amekubali hoja za upande wa mdai, kuwa suala la nani ashtakiwe na nani asishtakiwe ni jukumu la mdai kwa kuwa ndiye anaona kuwa nafuu anazoziomba atazipata kwa nani.

Amesema kesi hiyo haikuhitaji kutoa taarifa ya siku 90 kwa Serikali kwa kuwa si Serikali inayoshtakiwa bali kesi hiyo inahusu mgogoro wa ndani ya chama cha siasa, ambako Serikali haipaswi kujiingiza wala kuwa na upande.

Jaji Dyansobera amepanga kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo Desemba 8,2017 kwa kusikiliza hoja za msingi za mbunge Saleh na majibu ya wadaiwa na kisha atapanga tarehe ya kutoa uamuzi.

0 comments:

Wema Sepetu achoshwa....Atamani Kifo

Muigizaji mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amesema kuna muda anatamani Mungu amchukue afe ili aweze kupumzika na mambo ya dunia ambayo yanamnyima raha.

Wema Sepetu ameyasema hayo kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram, akisema ingawa anajua ipo siku atakufa, lakini anatamani ingetokea sasa ili aweze kupumzika na mambo yanayomuumiza nafsi yake ikiwemo kutukanwa bila sababu za msingi kwenye mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu amendeelea kusema kuwa kutokana na mambo ambayo anayapitia anatamani hata asingetokea duniani, na kuamua kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa muda.

"Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele... Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema...” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu... Ya Duniya ni mengi sana", ameandika Wema Sepetu.

Wema ameendelea kuandika akisema.." Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist... Ila acha niendelee kumtegemea yeye... Kila jambo hutokea kwa sababu.... Hili nalo litapita... I think I need a Time Off Social Media... Kwa mara nyingine Tena.... Siwezi jamani".

Licha ya hayo Wema Sepetu hajaweka wazi moja kwa moja ni jambo gani ambalo limemkwaza zaidi, kwani kitendo cha kutukanwa na kusemwa vibaya kwake sio jambo geni. 

0 comments:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 30



0 comments:

MKURUGENZI MKUU MSD AFANYA ZIARA HOSPITALI JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali wa Hospitali ya Sinza alipofanya ziara ya kikazi katika Hospitali hiyo na Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo, ili kubaini changamoto zilizopo za upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuzipatia ufumbuzi wa pamoja. Kutoka kulia ni Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola.
Maofisa wa Hospitali ya Sinza wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola, akizungumza katika mkutano huo.
Laboratory Manager wa Hospitali ya Sinza, Emmanuel Kiponda, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Sinza baada ya kufanya nao mazungumzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu, akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.


MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu amewatembelea wateja wa MSD wanaohudumiwa na Kanda ya MSD Dar e's Salaam ukiwa ni pamoja na Hospitali ya Mwananyamala na Sinza kubaini changamoto zilizopo katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ili kuzipatia ufumbuzi.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Jumanne jijini Dar es Salaam Bwanakunu amewataka wateja hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha Msd kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa Manunuzi maalumu.

Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

Akizungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na wamedata msaada wa magari kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu na changamoto kubwa ",alisema Bwanakunu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sinza, Chrispin Kayola alisema hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali hiyo kwa sasa ni asilimia 80 .

"Changamoto iliyopo ni uhaba wa vitendanishi vya maabara na vifaa vya macho na meno ambavyo tunapata chini ya kiwango hivyo havikidhi mahitaji tuliyonayo," alisema.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Daniel Mkungu alisisitiza haja ya ushirikiano baina ya Hospitali hizo na MSD ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Ziara hiyo ya mkurugenzi huyo itaendelea tena kesho katika baadhi ya hospitali zilizopo jijini Dar es Salaam
Na Dotto Mwaibale - Dar es salaam

0 comments:

Katibu Mkuu Chadema Wilaya ya Simanjiro ajiengua na Kuhamia CCM

Katibu wa Chadema Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Meshack Tureto amejiengua ndani ya chama hicho na kujiunga na CCM.

Tureto aliyekuwa pia katibu wa mbunge wa Simanjiro, James ole Millya ametangaza uamuzi huo akidai Chadema imepoteza dira na mwelekeo wa uongozi.

Anakuwa kiongozi wa pili wa Chadema wilayani Simanjiro kujiuzulu baada ya Jumamosi Novemba 25,2017 katibu wa uenezi, Ambrose Ndege kujiuzulu wadhifa huo na kujiunga na CCM.

Ndege alikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Tureto amesema amefikia uamuzi baada ya kuona viongozi wenzake hawana mikakati wala mipango ya maendeleo.

Tureto amesema awali, alikuwa mtendaji wa Kijiji cha Narakauwo kilichopo Kata ya Loiborsiret kwa tiketi ya CCM lakini aliacha na kufuata mabadiliko Chadema.

Amesema chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, mambo yanakwenda kama alivyotarajia hivyo hana sababu ya kuendelea kuwa Chadema.

"Chadema imepoteza mwelekeo sasa, nimeona nirudi CCM ambako hakuna kujilimbikizia vyeo na kila mwanachama ana haki kwa kuwa hii ni CCM mpya," amesema Tureto.

Amesema hakuingia Chadema kwa lengo la kupata masilahi bali alijiunga kwa utashi wake kama ambavyo sasa ameondoka na kurudi CCM.

Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya amemtakia Tureto heri anakokwenda. Amesema sababu alizotaja za kuondoka Chadema hazina mashiko.

Ole Millya amesema Tureto aliingia Chadema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 baada ya kuona yeye ana nafasi kubwa ya kuwa mbunge wa Simanjiro.

Amesema Tureto alikuwa mtendaji wa Kijiji cha Narakauwo na alifukuzwa hivyo aliomba apatiwe nafasi naye akamjibu hana sifa.

Ole Millya amesema Tureto hakuwa katibu wa Chadema aliposhinda ubunge mwaka 2015 bali Frank Oleleshwa ambaye miezi sita iliyopita alipojiuzulu ndipo naye akashika nafasi hiyo.

"Wengi wanatafuta mafanikio binafsi na utajiri, lakini ukweli utabaki palepale CCM haitatawala milele Tanzania," amesema Ole Millya.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Jackson Sipitieck amempongeza Tureto kwa kujiunga na chama hicho na amemhakikishia ushirikiano wa kutosha.

0 comments:

TANESCO YAKANUSHA UVUMI UNAO ENDELEA

KANUSHO: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekanusha taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikiwataka wateja kununua umeme kwa wingi kutokana na zoezi linaloendelea la kubomoa Ofisi za Makao makuu yake, Ubungo linalodaiwa kuathiri mfumo wake wa LUKU.

“Tunaomba wateja wetu wapuuze taarifa hiyo, kwani TANESCO kama ilivyobainisha katika taarifa ya awali, huduma zote za umeme ikiwemo ya manunuzi ya LUKU zitaendelea kama kawaida .Tutaendelea kutoa taarifa kila inapohitajika.”

Azam TV

0 comments:

TANESCO Wataja Chanzo cha Kukatika kwa Umeme Dar, Pwani

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na hitilafu iliyojitokeza.

Taarifa ya Tanesco imesema baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo hayana umeme kuanzia saa 3:20 asubuhi ya leo Jumatano Novemba 29,2017 kutokana na mashine namba tatu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia kituo cha Ubungo II kupata hitilafu.

“Mafundi wa shirika wanaendelea na jitihada za kutatua hitilafu hiyo kwa haraka ili kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida,” imesema taarifa ya Tanesco.

Shirika hilo limesema litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo.

Pia, Tanesco imetoa tahadhari kwa wananchi kutosogelea, kushika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Uongozi wa shirika hilo umewaomba radhi wateja kwa usumbufu uliojitokeza

0 comments:

Waziri Mkuu Abaini Semi Trela 44 Zikitaka Kutolewa Bandarini Bila Yakufuata Utaratibu....Amtaka IGP Sirro Awakamate Wahusika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.

“Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.”

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 29, 2017) alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.

Hatua hiyo imekuja baada ya Bw. Bahman wa kampuni ya NAS kutaka kupata msamaha wa  kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kwamba wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata matatizo.

Amesema Serikali inasisitiza watu kufuata sheria na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kulipakodi  ipasavyo na inataka watendaji wake wafanye kazi bila ya kubugudhiwa, hivyo amewataka wafanyabiashara kufuata sharia za nchi na kwamba Serikali haina ugomvi nao.

Waziri Mkuu amefafanua kuwa mfanyabiashara huyo alitaka kuyatoa magari hayo bila ya kukamilisha malipo ya ununuzi kutoka kwenye kampuni Serin ya nchini Uturuki.

“Magari haya aliyalipia asilimia 30 tu kwa makubaliano ya kumaliza asilimia 70 iliyobaki baada ya kufika Tanzania na atakapokamilisha ndipo angepewa nyaraka ambayo inaonyesha jina la mwenye mzigo, aina ya mzigo na thamani  (bill of lading) inasaidia mteja kufanyiwa tathmini ya gharama za kulipia ushuru, lakin huyu bwana hajafanya hivyo”

Waziri Mkuu amesema kitendo cha kuyasajili magari hayo bila ya kuwa na nyaraka hizo ni kinyume cha sheria na pia kinaweza kusababisha kampuni iliyouza magari hayo ya Serin kutolipwa malipo yaliyobaki. 

Amesema jambo hilo halikubaliki kwa sababu linaweza kudhohofisha mahusiano mazuri iliyopo kati ya Tanzania na Uturuki kwani tayari kampuni hiyo imeshawasilisha malalamiko hayo katika ofisi za Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania.

“Uturuki wanawaamini sana wafanyabiashara wa Tanzania sasa huu ujanjaunja uliotumika katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuyasajili magari haya bila ya kuwa na bill of lading halisi unajenga sura mbaya kwa wafanyabiashara wengine waaminifu na watiifu wa sheria nawaagiza TRA kuchukua hatua kwa wahusika, hatuwezi kupoteza mahusiano na nchi kwa sababu ya utapeli wa mfanyabiashara mmoja.”

Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Mawakala wa Forodha kuhakikisha wanakuwa makini katika kazi zao na Serikali haitawavumilia wababaishaji kwani inasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.

Awali, Mkurugenzi wa Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alimueleza Waziri Mkuu kuwa pamoja na vitisho vya mfanyabiashara huyo kuwa wasipotekeleza matakwa yake watapata matatizo, lakini waliendelea kusimamia sheria na taratibu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, NOVEMBA 29, 2017

0 comments:

IGP Sirro Asema mtandao Wa Kiuhalifu Kibiti Umesambaratishwa Kwa Kiasi Kikubwa....Ataka Watoto 13000 Wapatikane Haraka

MKUU wa jeshi la polisi nchini (IGP)Simon Sirro amewahakikishia wananchi mkoani Pwani kuwa silaha zote zilizochukuliwa na wahalifu wa ovyo ovyo huko Kibiti na Mkuranga zimerudi zote mkononi mwa dola na kusambaratisha mtandao wa kiuhalifu .

Aidha ametoa rai kwa wazazi na walimu kutoa taarifa kwenye vituo vya polisi mara watakapobaini kuna mwanafunzi mtoro ama hajaripoti shule kwa miezi kadhaa kwani wapo baadhi ya watoto wanaotumika kufundishwa uhalifu hata wakutumia silaha na watu wasiowema.
 
Pamoja na hayo IGP Sirro ,amesema vyombo vya ulinzi na usalama nchini vinashirikiana na nchi ya Msumbiji kupambana na wahalifu waliobainika kukimbilia nchini  humo wakitokea Tanzania.
 
Aliyasema hayo wilayani Kibaha ,mkoani Pwani ,katika ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo pia alizungumza na viongozi wa mashirika ya umma,wazee maarufu ,wastaafu mbalimbali na kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo.
 
IGP Sirro alieleza kuwa ,vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kupambana na yeyote atakaekuja kwa moto nae wataenda nae kwa moto na atakaekuja baridi wataenda nae baridi.
 
Alisema serikali imeshinda kwa hilo na hali kwa sasa ni shwari katika wilaya hizo.
 
IGP Sirro alieleza amepatiwa taarifa ya wanafunzi zaidi ya 1,300 mkoani hapo kuwa ni watoro na hawajulikani walipo hivyo wazazi washirikiane kusaidia jeshi la polisi kujua walipo.
 
“Kuna baadhi misikiti,makanisa yanadaiwa yanayotumia watoto hawa katika masuala ya kiuhalifu hivyo kuna kila sababu ya kuingia ndani kutafuta suluhu “
 
“Ni kazi yetu wazazi jamii na walimu kushirikiana ,na hapa ni muhimu wazazi wasaidie kusema watoto wao walipo ili kuwa na usalama” alisema .
 
Katika hatua nyingine IGP Sirro alielezea viongozi wa dini wana nafasi ya kuhakikisha wanatumia eneo lao kuhubiri amani .
 
“Tusidharau taarifa hata kama ni ndogo ,tusibweteke umoja ni nguvu tusaidiane kukomesha vitendo vya uvunjifu wa amani ” alifafanua IGP Sirro.
 
Akizungumzia changamoto ya wahamiaji haramu alisema wanashirikiana na uhamiaji kuusaka mtandao unaohusika kufanya biashara ya kusafirisha wahamiaji haramu .
 
IGP Sirro alisema hawatamvumilia yeyote anaekumbatia wahamiaji haramu kwani ni chanzo cha kusababisha kuleta magaidi  na kusafirisha bidhaa za haramu .
 
Alisema kwasasa wamejipanga kutaifisha mali za wafanyabiashara hao wa wahamiaji haramu na usafiri utaotumika kuwasafirisha.
 
Nae mkuu Wa Mkoa Wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,ameshukuru kuwepo Kwa kanda maalum kwani imeweza kuleta mafanikio makubwa .
 
Alisema kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya sintofahamu ,watu walisitiza shughuli zao za maendeleo ,biashara zilikwama,watu na baadhi ya viongozi walihama nyumba zao na wengine kulala saa 12 jioni kwa kuhofia mauaji.
 
Mhandisi Ndikilo alieleza sasa Kibiti na Rufiji hali ni shwarii kutokana na kuimarishwa ulinzi.
 
Aliwataka pia wawekezaji na wadau mbalimbali mkoani Pwani ,kujitokeza kushirikiana kusaidia kutatua changamoto zinazolikabili jeshi la polisi ikiwemo uhaba wa vitendea kazi ,usafiri na kujenga vituo vya polisi .
 
Mhandisi Ndikilo, alisema kuwa Mkoa huo umesheheni viwanda vya kutosha hivyo ni vyema kusaidia mambo hayo kwa manufaa ya wote wakati kukitokea uhalifu.
 
“Tukikumbwa na uhalifu tunapigia simu polisi, tusiwe Wa kwanza kulaumu wakati wa matatizo ,tukumbuke na kuwasaidia ili kufanikisha kazi zao kifanisi.;:” alisema mkuu huyo wa mkoa .
 
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Pwani ,(ACP)Jonathan Shanna alisema ziara hiyo ni neema kwao na wamepewa maagizo mbalimbali ambayo watayafanyia kazi.
 
Kamanda Shanna alisema wamemfikishia kero IGP zinazowagusa askari polisi ikiwemo upungufu wa makazi .

0 comments:

MANULA, KICHUYA WAPEWA NJUMU ZA SH 500,000

NYOTA wawili wa kutumainiwa wa klabu ya Simba, Mlinda mlango Aishi Manula pamoja na kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya, wamepokea viatu vyenye thamani ya Sh 500, 000 kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.

Wawili hao walikabidhiwa viatu hivyo aina ya CR7 Mercurial kutoka kampuni ya Nike, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli, ulioisha kwa sare ya bao 1-1 uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa viatu hivyo, Manula alisema anajisikia fahari kupata zawadi hiyo kutoka kwa mashabiki hao ambao wameonyesha upendo wao kwake na kuahidi kuendelea kufanya vizuri ili kuwafurahisha zaidi.

“Ni jambo zuri ambalo linatia hamasa ya kuendelea kujituma zaidi na kuisaidia timu kufanya vizuri zaidi katika michezo ya ligi kuu ili tuweze kutimiza malengo yetu,” alisema.

Naye Kichuya alisema zawadi hiyo itakuwa chachu kwake kufanya vizuri zaidi kutokana na upendo anaoonyeshwa na mashabiki hao, ambao wamekuwa wakiwaunga mkono katika harakati zao za kulisaka taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara

0 comments:

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa apokea vifaa vyya mshindano ya majimbo vyenye thamani ya Tsh 50 milioni.





0 comments:

Korea Kaskazi Yarusha Kombora La Masafa Marefu Zaidi Linaloweza Kutua Sehemu Yoyote Duniani




Korea Kaskazini imelifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kudumu angani kwa dakika 53 kabla ya kutua katika bahari ya Japani.

Kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis,kombora hilo ni hatari zaidi kwa sababu liweza kutua katika kona yoyote ile ya dunia ikiwemo Marekani.

Komora hilo liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960kulingana na jeshi la Korea Kusini.

Mara ya mwisho kwa  taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba. Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo.

Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya vikwazo ilivyowekewa.

Baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya kombora lililorushwa jana.

Rais wa Marekani Donald Trump aliarifiwa kuhusu hatua hiyo wakati ambapo kombora hilo bado lilikuwa angani  ambapo aliishia tu kusema ''Tutalishughulikia''.

0 comments: