Mkurugenzi
wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB), Abdul Razaq Badru amesema
kuwa bodi hiyo itafungua dirisha la kukata rufaa kwa wanafunzi waliokosa
mikopo ili waweze kupata haki yao.
Ameyasema
hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifafanua vigezo na sifa za
mwanafunzi kupata mkopo baada ya kuwepo kwa kasoro kadhaa kwa baadhi ya
waombaji katika awamu ya kwanza ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
“Kwa
wale wenye changamoto ndogo ndogo labda walikosea, tutatangaza dirisha
la kukata rufaa mapema wiki ijayo na tutashughulikia watakaokamilisha
vigezo watapata mkopo lakini wanatakiwa kuzingatia maelekezo
tutakayoyatoa,” amesema Badru
Hata
hivyo, mkurugenzi amesema katika majina ya waombaji waliyoyapokea na
kuthibitishwa na TCU kwamba yamepata vyuo na wakayapitia wakajiridhisha
hayana kasoro kwenye uombaji, tayari wanafunzi 29,578 wameshapata mkopo
na wameanza masomo ambapo kiasi cha shilingi bilioni 96 zimetumwa vyuoni
0 comments: