KAMA ILIKUPITA BASI USILALAMIKE.......
BAADA YA SOMALIA KUPATA RAIS MPYA: Mambo usiojua kuhusu rais mpya wa Somalia
Ana uraia wa nchi mbili za Marekani na Somalia na anajulikana kwa kampeni yake ya kupigania haki za kibinaadamu.
Amewahi kuhudumu kwa muda mfupi kama waziri mkuu mwaka 2011 lakini akajiuzulu baada ya miezi michache kufuatia migogoro kati yake na aliyekuwa rais Sheikh Sharrif hassa.
Hakuwa maarufu na wanasiasa wengine kwa kuwa alijionyesha kuwa mtu wa watu akipanda ndege za bei ya chini wakati alipokuwa akisafiri katika mataifa ya ughaibuni.
Miongoni mwa wagombea wote 20 ndiye aliyekuwa maarufu katika mtandao wa kijamii.
Wapinzani wake walikosolewa kwa kuungwa mkono na Kenya na hata Ethiopia.
Wafuasi wake wanapinga mataifa ya kigeni kuingilia kati utawala wa Somalia na wanataka kuona mabadiliko nchini humo
KUELEKEA UBUNGE WA AFRIKA MASHARIKI
UBUNGE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI: WATANZANIA WATAKIWA KUTOA MAONI
kwa mtazamo wako nani anastahili kuwa mbunge na nani hastahili?, ili kutoa maoni yako hayo juu ya mtu unayetaka au unayehisi anastahili kuwa mbunge wa Bunge lijalo la Afrika mashariki tafadhali Tuma email yako katika anuani yetu ya EMAIL: jamvilahabari@gmail.com
nasisi tutakusanya matokeo yote na kuyatoa kwa umma
HAWA HAPA MARAIS WA KWANZA AFRIKA KUZUNGUMZA NA TRUMP
NI ZUMA NA BUHARI, MARAIS WA KWANZA WA AFRIKA WALIOZUNGUMZA NA TRUMPAT
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari leo
hii akiwa mjini London amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Marekani
Donald Trump, kufuatia ombi kutoka kwa rais huyo wa Marekani.
Viongozi hao wawili walizungumzia njia za kuboresha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.
Trump alimshauri Rais Buhari kuendelea na kazi nzuri anayoifanya na pia kumpongeza kwa jitihada alizofanya za kuokoa wasichana 24 wa Chibok na hatua zinazopigwa na jeshi la Nigeria.
Trump alimhakikishia rais huyo wa Nigeria kuwa Marekani iko tayari kuafikiana na Nigeria kuhusu suala la kuisaidia na silaha ili iweze kukabiliana na ugaidi.Rais Trump pia amemualika Buhari kwa ziara nchini Marekani.
Baadaye Trump pia alifanya mazungumzo ya simu na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Viongozi hao walikubaliana kufanya jitihada za kuboresha zaidi ushirikiano mzuri uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Zuma alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.
Kunazo kampuni 600 za kimarekanai nchini Afrika Kusini na pia ushirikiano mzuri wa kibiashara kati ya mataifa hayo.
Marais hao pia walijadili umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala kadha ya kuhakikisha kuwepo amani barani la Afrika.
SIASA ZA KENYA: Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Mwakwere ajiuzulu
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere amejiuzulu.
Bw
Mwakwere, ambaye amekuwa balozi wa Kenya katika nchi hiyo jirani tangu
mwanzoni mwa mwaka 2015, alijiuzulu rasmi Ijumaa kumuwezesha kuwania
katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.Watumishi wa umma kikatiba wanafaa kujiuzulu kufikia 15 Februari.
Bw Mwakwere, ambaye mwishoni mwa wiki alitangaza rasmi kuhamia chama cha upinzani cha ODM, alikuwa awali mwanachama wa chama cha URP, moja ya vyama vilivyounda muungano wa Jubilee ulioshinda uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Aliwania wadhifa wa seneta katika uchaguzi huo lakini akashindwa na Boy Juma Boy wa chama cha ODM.
Bw Mwakwere ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kuwania wadhifa wa ugavana katika kaunti ya Kwale, baada ya gavana wa sasa Salim Mvurya kuhama chama cha ODM na kujiunga na chama Jubilee chake Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto.
"Nimekuwa balozi, wadhifa muhimu sana wa kutumikia maslahi ya wananchi wa Kenya katika ngazi ya kibalozi. Kazi yangu sasa ni kuimarisha hali ya maisha ya watu wa Kwale," alisema Jumapili, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.
"Ninataka kuweka mambo wazi, nimejiondoa chama cha Jubilee na sasa niko na watu wangu katika National Super Alliance (muungano wa wagombea wa upinzani."
Mwakwere, 71, alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Kenya kati ya 2004 na 2005 na baadaye akateuliwa waziri wa uchukuzi Desemba 2005.
Alipoteza wadhifa wake wa uwaziri Februari 2010 baada ya kushindwa katika kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake kama mbunge wa Matuga lakini alishinda uchaguzi wa marudio baadaye mwaka huo dhidi ya mpinzani wake Hassan Mwanyoha.
TRA Yakusanya Sh Trilioni 8.4 Kwa Miezi Sita
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh trilioni 8.41 kuanzia Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu
kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, inaonesha makusanyo ya Januari mwaka huu
ni Sh trilioni 1.14.
Kayombo alisema
pamoja na juhudi za kukusanya kodi mbalimbali, hivi sasa wameelekeza
nguvu katika kukusanya kodi ya majengo kwa kutoa ankara kwa wamiliki wa
majengo katika mikoa mbalimbali.
“Wamiliki wa
majengo wanakumbushwa kwamba kodi ya majengo inakusanywa na TRA kuanzia
Julai mwaka jana, hivyo tunawaomba watoe ushirikiano kwa kulipia ankara
zao kwa wakati,” alisema Kayombo.
KAmati Kuu ya CHADEMA Yabariki Mbowe Amshitaki Makonda kwa Kumdhalilisha
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimejipanga na kitampatia
mawakili wa chama Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe katika hatua yake ya
kumfungulia kesi ya kikatiba na ya madai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda.
Februari 8
mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitaja majina 65
kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya akiwamo Mbowe
na kuwataka kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya
kuhojiwa.
Lakini siku
moja baadaye Mbowe aliitisha mkutano na waandishi wa habari akiwa mjini
Dodoma ambapo alieleza kutofika polisi kwa wito wa Makonda akisema hana
mamlaka hiyo isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
Mbowe ambaye
pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni aliweka bayana nia yake ya
kumfungulia mashtaka ya madai Makonda kwa kumkashifu na kumchafulia
jina.
Akitoa maazimio
ya kikao cha kamati ndogo ya Kamati Kuu ya Chadema jijini Dar es Salaam
jana, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdalah Safari alisema
kamati hiyo inaunga mkono hatua ya Mbowe kumfungulia kesi ya kikatiba
Makonda.
“Katika hili
tumejipanga kweli kweli…tutaungana na Mbowe katika kesi hii na
tutampatia mawakili wa chama akiwamo mimi na tuko wengi,”alisema.
Profesa Safari
aliwataka wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa kujihusisha
na biashara au utumiaji wa dawa za kulevya wafungue mashauri mahakamani.
“Tunatoa
wito kwa wale wengine wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa,
kuchafuliwa majina na au kudhalilishwa wafungue mashauri mahakamani,
kwani hii ndio njia pekee ya kuzuia wengine wasifanyiwe uonevu kama huu
siku zijazo,”alisema Profesa Safari.
Pamoja na mambo
mengine, Profesa Safari alisema tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu 2015
viongozi na wanachama wa Chadema wamekuwa wakikamatwa na kushtakiwa kwa
makosa ya kubambikiziwa kwa kisingizio cha uchochezi.
Alisema mpaka sasa jumla ya wanachama na viongozi 215 wamefunguliwa kesi zaidi ya 78 nchi nzima.
“Kati ya hao
wengi wao wamenyimwa dhamana bila sababu za msingi huku wale ambao
walipatikana na hatia walipewa adhabu za vifungo bila kupewa fursa ya
faini.
“Kutokana na
hilo, hivi sasa tunaandaa orodha kamili itakayoainisha kesi zote za
jinai ambazo ziko mahakamani na kuonyesha aina ya mashtaka na vifungo
vilivyotolewa ambayo itawekwa wazi kwa vyombo vya habari na taasisi za
ndani na nje ya nchi kuthibitisha kuwa kuna mpango wa kuwafunga viongozi
wa upinzani kwa kusudi ili kuwadhoofisha,”alisema Profesa Safari.
Katika hatua
nyingine Profesa Safari aliwaomba marais wastaafu, mawaziri wakuu
wastaafu na majaji wastaafu kuzungumza na Rais John Magufuli kutokana na
yanayoendelea na kwamba wasiogope kwani wao hawatatumbuliwa.
“Marais
wastaafu Ali Hassani Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wanaogopa
nini? Kwanini wasimwambie Rais Magufuli kuwa na wao waliapa kuilinda
Katiba ya nchi hivyo na yeye afanye hivyo.
ZITTO KABWE NA KUFUNGIWA KWA WIMBO WA NICK MBISHI
Afunguka kuhusu kufungiwa kwa wimbo ‘I’m Sorry JK’ wa Nikki Mbishi
Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK umefungiwa.
Uamuzi huo
umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa la
Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia
Instagram, Nikki amewaonya watu dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa
mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba
niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa
ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na
hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram.
“Napokea
simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa
watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba
nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa
yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi
sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na siwezi
kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili
usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu
mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.”
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook:Serikali
imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni
utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”
FAHAMU ZAIDI JUU YA TISHIO LA KUFUTWA TLS
TUNDU LISSU AMVAA MWAKYEMBE SAKATA TLS
Waziri wa
Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe jana alisema kuwa atakifuta
Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society (TLS)) kwa madai
kuwa kimesahau misingi yake na kuanza kufanya kazi kama chama cha
siasa.
Waziri
Mwakyembe alisema kuwa, kama wanataka kufanykazi kama chama cha siasa,
basi yeye ataongea na msajili wa vyama vya siasa nchini ili cha hicho
kipya kisajiliwe.
Kufuatia kauli
hiyo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki na
mgombea Urais wa TLS, Tundu Lissu ameandika waraka huu kwenda kwa
wanasheria wenzake.
Mawakili
wenzangu. Mimi binafsi sijashangazwa na kauli ya Dkt. Mwakyembe kwamba
ataifuta TLS kama itajiingiza katika harakati za kisiasa. Hii sio mara
ya kwanza kwa viongozi wa serikali ya Tanzania kutoa vitisho vya kuifuta
TLS.
Waziri Mkuu
hayati Edward Sokoine aliwahi kutishia hivyo katika kilele cha vita
dhidi ya wahujumu uchumi miaka ya mwanzo ya ’80. Na hata kabla ya hapo
katika miaka ya ’60 na ’70 watangulizi wa Sokoine walijaribu kufanya
hivyo hivyo. In fact, kuanzishwa kwa Tanzania Legal Corporation kipindi
hicho kulikuwa driven in part na jitihada za kuondoa the private bar.
Vitisho dhidi
ya TLS vilirudi miaka ya ’90 wakati wa Lyatonga Mrema. Kitu kimoja kiko
common katika vitisho hivyo vyote. Vitisho hivi vimetolewa kila wakati
TLS na private bar wanapo-assert their independence na wanapoanza
kutetea utawala wa sheria na kupinga state lawlessness and impunity of
the rulers.
Mawakili wakiwa
kimya na TLS ikiwa mfukoni mwa serikali na wasipohoji matumizi mabaya
ya madaraka basi wanakuwa darlings wa serikali.
Kuna kitu
kingine ambacho ni common katika vitisho hivi. Havijawahi kufanikiwa na
havitafanikiwa. Sheikh Abeid Amani Karume alipiga marufuku private legal
practice mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya ’64. Tanzania ya leo
sio Zanzibar ya miaka ya ’60 na ’70, hatutakubali udikteta wa aina ya
Karume au wa aina nyingine yoyote kwenye Tanzania ya leo.
Inaelekea Dkt.
Mwakyembe hafahamu au anajisahaulisha jinsi ambavyo TLS na mawakili
binafsi walivyo embedded kwenye mfumo wetu wa kikatiba na kisheria.
Simply put, ukifuta TLS maana yake ni kwamba hakuna wakili binafsi hata
mmoja nchi nzima. Mfumo mzima wa kimahakama unategemea uwepo wa mawakili
na kwa hiyo uwepo wa TLS. Mahakama karibu zote zitashindwa kufanya kazi
kusipokuwa na mawakili binafsi. The same applies to various tribunals
and other judicial and quasi judicial bodies.
Aidha, kuna
taasisi nyingi zilizoundwa na Katiba yetu kama vile Judicial Service
Commission na Law Reform Commission ambazo zinakuwa properly constituted
kukiwa na uwakilishi wa TLS. Kuna taasisi nyingine nyingi ambazo
zimeanzishwa na sheria za kawaida ambazo composition yake inakamilika
kukiwa na representation ya TLS. Hiyo legal, constitutional and
political upheaval itakayotokana na kufutwa kwa TLS will be
unprecedented and unimaginable kwa mtu mwenye akili timamu.
Dkt. Mwakyembe
ana akili timamu. He must be joking. Hawezi kufuta TLS. Anachotaka
kufanya ni kuwatisha mawakili ili wachague watu wale wale wa miaka yote
kuongoza TLS. Anatutisha ili tuendelee na status quo katika uongozi wa
TLS. Hataki tufanye mabadiliko yanayohitajika ili TLS yetu isichukue
nafasi yake stahiki katika kuamua mustakbala wa nchi yetu na wa taaluma
yetu.
Nawataka
viongozi na wanachama wa TLS wamkemee Dkt. Mwakyembe in the strongest
possible terms. Nawataka wagombea wenzangu wa nafasi mbali mbali za
uongozi katika TLS wajitokeze hadharani na kulaani kauli ya Dkt.
Mwakyembe in no uncertain terms. Wakinyamaza tutawajua wako upande wa
nani: status quo au mabadiliko. And I’ll ask you all to vote
accordingly.
WASSIRA, BULAYA BADO NGOMA MBICHI
Wafuasi wa Steven Wassira Waendelea Kumng'ang'ania Ester Bulaya....
Wapigakura
wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi
Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester
Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maombi
yao.
Msajili wa
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alisema jana kuwa rufaa ya
wapigakura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Acetic
Malagila iliyosajiliwa kwa namba 199 ya mwaka 2016, itasikilizwa
mfululizo kuanzia Februari 20.
Alisema rufaa
hiyo itasikilizwa jijini Mwanza na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya
Rufani, Salim Mbarouk, Augustine Mwarija na Shabani Lila.
Katika maombi
ya msingi waliyofungua Mahakama Kuu, wapigakura hao wanaowakilishwa na
Wakili Constantine Mutalemwa, wanaiomba Mahakama kutengua ushindi wa
Bulaya dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Stephen Wasira kwa madai kuwa
uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka 2015 haukuwa huru na wa haki.
Pamoja na madai
mengine, Masato na wenzake wanadai kuwa mchakato wa kampeni, upigaji
kura na utangazaji wa matokeo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria na
utaratibu wa uchaguzi, vikiwamo vitendo vya rushwa, msimamizi wa
uchaguzi kumnyima haki Wasira kwa kukataa ombi lake la kura kuhesabiwa
upya.
Hoja nyingine
ni msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo bila Wasira kuwapo ukumbini
na kuchanganya tarakimu za idadi ya wapigakura walioshiriki uchaguzi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments: