0 comments:

Barcelona Wanamtesa Messi Waliyeamini Ataishi Milele.

ATHUMAN BEMELENGO - DAUDA.COM
0713 094952
Majuma kadhaa yaliyopita nilipata kuwatazama wachezaji wawili bora zaidi kwasasa ulimwenguni. Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Nilimuona Messi aliyecheza dhidi ya Juventus ambaye kimsingi hakucheza kwa kiwango bora. Pia nilimuona Ronaldo aliyecheza dhidi ya Bayern Munich.

Unaweza kusema walikuwa binadamu tofauti sana na wale tuliozoea kuwaona kila mmoja kwa michezo waliyocheza. Lakini ndio uhalisia. Messi dhidi ya Juventus alikuwa mchezaji wa kawaida sana ambaye usingeweza kuamini kama ndio yeye kama ndio ingekuwa mara ya kwanza kumuona baada ya kusimuliwa maajabu yake.

Cristiano Ronaldo yeye alikuwa na usiku mzuri dhidi ya Bayern Munich baada ya kuiwezesha timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali dhidi ya timu bora kama Bayern Munich tena akiwa amefunga magoli matano katika michezo yote miwili. Sio kitu rahisi kufunga magoli matano mbele ya kipa mwenye kiwango cha Manuel Neuer.

Ulikuwa usiku pekee ambao ungeweza kumpata mshindi katika ile debate ya ubora wa hawa wafalme wawili. Mtizame Ronaldo, licha ya kuwa na umri mkubwa lakini anaonekana bado ana uwezo mkubwa wa kucheza na kufunga tofauti na Messi ambaye anaonekana kabisa kasi yake imepungua.
Kabla ya El Classico ungeweza kuamini Messi hana jipya tena zaidi ya ndevu zake kuwa maajabu pekee aliyobakiza. Huu ndio ulikuwa wimbo wa wale waliomdhihaki.

Niliulizwa sana, Ni kweli Messi alikuwa ameisha? Jibu sahihi lilikuwa hapana, Nikaulizwa tena, sasa tatizo ni nini? Na kwa nini Ronaldo licha ya kuwa na umri mkubwa zaidi anaonekana kuwa bora?
Hayo ni baadhi ya maswali niliyoulizwa na waliotaka kujua kwa nini nilikuwa nikisema Messi bado hajaisha na anaweza kuendelea kuwa mshindani sahihi wa Ronaldo wakiitafuta pensheni yao.

Suala ni moja tu, Ronaldo kwa upande wake yeye amejua namna sahihi ya kucheza kwa wakati huu ambao umri umeanza kumtupa mkono. Ronaldo wa sasa hivi hakimbii sana wala hakai sana na mpira. Unaweza usimuone timu ikicheza mpira na ukalazimika kumuona akifunga tu.

Analazimika kugusa mpira mara chache sana hasa pale inapobidi. Real Madrid tayari inao watu wanaoweza kumfanya Ronaldo asilazimike kuuchezea zaidi mpira na akasubiri tu mbele ya goli la timu pinzani ili afunge.
Miguu ya Toni Kroos na Luka Modric inafanya kazi kubwa kuhakikisha inautawanya mpira katika maeneo yote ya uwanja huku Marcelo na Carvajal wakiwa na jukumu la kupeleka mipira salama kwa Ronaldo.
Hivi ndivyo Real Madrid ilivyojiandaa kumfaidi zaidi Ronaldo akiwa anaelekea katika uzee wake. Unafikiri hawakuujua umri wake walipoamua kumpa mkataba mrefu mpaka mwaka 2022? Hawezi kuwa Florentino Perez anayeweza kufanya biashara ya kiuendawazimu.

Wanaweza kuwatumia Isco na James Rodriguez ili Ronaldo apate muda wa kupumzika. Hii ndio njia sahihi ya kuwatumia wachezaji walioanza kuishi mbali na zama zao. Hawahitaji kukimbia sana uwanjani, kufanya kazi nyingi uwanjani au kucheza muda mrefu bila kupumzika.

Madrid tayari wanalijua hili na wameshaona wamefanikiwa na ndio maana wanapata jeuri ya kuamini hawana haja ya kutumia nguvu nyingi kuzipata nyayo za Eden Hazard kuliko mikono salama ya David De Gea.

Ukimuangalia Messi unaweza kudhani ni mkubwa kuliko Roaldo lakini shida yake ameanza kutumika mapema sana. Akiwa na miaka 19 alishaingia katika rekodi ya kufunga hat trick kwenye El Classico.Barcelona wamejisahau sana.

Waliamini kile kizazi alichokitengeneza Pep Guardiola akiwa kocha wa vijana pale Catalunya kingeishi milele. Hakuna kizazi kilichoandaliwa kuja kurithi zama zao.Messi anahitaji kupumzika, kuugusa mpira mara chache katika maeneo hatari zaidi na akiwa hakimbizani tena na mabeki.

Lakini mambo ni tofauti sana. Barcelona ya sasa inamhitaji zaidi Messi kuliko unavyofikiri. Matokeo yake wamemfanya kuwa mtumwa, anateseka sana. Wanamhitaji afunge, aichezeshe timu na ikibidi akabe pia. Unampata wapi tena Messi anayeweza kufanya yote haya wakati hata yule wa ubora wake hakuweza.

Barcelona haina tena mashine zake zilizoifanya kuwa tishio kuanzia kwenye eneo la kiungo. Sergio Bosquets na Andres Iniesta tayari wamejichokea. Huwezi tena kuziona miguuni mwao zile  pasi zilizomtia ‘Degedege’ Sir Alex Ferguson pale Wembley mwaka 2011. Ni vijana wa kiume pekee walioweza kumtetemesha mwanaume Sir Alex Ferguson.

Ni nani anaweza kuifanya ile kazi aliyokuwa akiifanya pass master Xavi Hernandez ambaye alikuwa na uwezo wa kukimbia uwanja mzima akiwa amepiga pasi nyingi zaidi ya timu pinzani?
Sio Ivan Rakitic wala Andre Gomes anayeweza hata kujaribu ila inabaki kuwa kazi nyingine ya Lionel Messi. Unaikumbuka mechi dhidi ya PSG? Luis Enrique alimuanzisha Messi katika eneo la kiungo kuifanya kazi hii huku Rafinha akianzishwa katika safu ya ushambuliaji sambamba na Neymar na Luis Suarez.

Siku ile Messi alikuwa mtu muhimu zaidi uwanjani huku Neymar akiwa mchezaji bora. Sio Iniesta wala Rakitic ambaye angeweza kuwashinda Verrati na Rabiott pale kati ya dimba.Ulimuona Messi dhidi ya Real madrid?
Kupitia kwake utakiona nilichokueleza hapo juu. Alihitajika kumsaidia Iniesta katika eneo la kiungo ili kuiunganisha timu kutoka eneo la kiungo hadi mbele. Ilikuwa kazi rahisi sana kwa uwezo wake. Alimaliza mechi akiwa ametimiza magoli 500 ya La liga na magoli 23 aliyofunga kwenye El Classico.

Messi bado ana uwezo wa kuendelea kucheza kwa muda mrefu tena kwa kiwango kikubwa hata zaidi ya Cristiano Ronaldo kama Barcelona watatafuta namna sahihi ya kumtumia kwa kipindi hiki ambacho anaonekana umri umeanza kuachana na kasi yake.

Njia pekee na sahihi ni kuijenga timu upya itakayomhitaji Messi kutumia zaidi akili yake na ubunifu kufunga magoli bila kutumia nguvu kubwa. Kama wataona hawahitaji kufanya hivyo kutokana na uwepo wa Neymar, basi watakuwa wanajiongopea.

Nani ataweza kuutawanya mpira katika maeneo yote ya uwanja kama walivyokuwa wakifanya Xavi na Iniesta? Neymar pekee? Hatoweza kuifanya hata anayoifanya Messi sasa hivi.
Wanahitaji damu changa kama Thiago Alcantara na Marco Verrati au Hector Bellerin bila kusahau watu imara katika safu ya ulinzi.

Ukiwa na watu wa aina hii, ni lini Messi atalazimika kushuka kwenye  eneo la kiungo kukimbizana? Hii ndio njia sahihi itawafanya Barcelona waendelee kumfaidi Messi kwa muda mrefu zaidi.

0 comments:

MKUU WA MKOA WA MWANZA AHITIMISHA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, KITAIFA JIJINI MWANZA



29

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza.
Mongella amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.
Amewahimiza zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano.
#BMGHabari

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.

Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan, akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.

0 comments:

BREAKING NEWS: Mtandao wa Whatsapp umepotea hewani dunia nzima



Inawezekana wewe ukawa ni mmoja kati ya watu ambao wameshangazwa na kuona simu zao usiku huu ukituma ujumbe wa Whatsapp hauendi na kuanza kujiuliza kama shinda ni salio, simu au tatizo la kiufundi.

Taarifa ikufikie kuwa tatizo hilo limetokea na kwa mujibu wa msemaji wa mtandao huyo” baadhi ya watu wamepata tatizo la kushindwa kupata huduma ya whatsapp kwa leo, tunaomba radhi kwa usumbufu na tunashughulikia kuhakikisha huduma hiyo inarejea mapema”

SOURCE: express.co.uk
BREAKING: Mtandao wa Whatsapp hauko hewani dunia nzima sababu za kutokuwa hewani bado hazijawekwa wazi kama tatizo nini

0 comments:

Ulipofikia ujenzi wa Daraja la Furahisha, Mwanza


Kila siku Jiji la Mwanza linakuwa kwenye muonekano mpya kuanzia kwenye majengo, barabara mpaka kwenye madaraja ambapo ukiachana na daraja la Mabatini, kuna Daraja jipya ambalo linaendelea kujengwa eneo la Furahisha.

Ni daraja mbalo kwa chini linaruhusu magari kupita pamoja na pikipiki na juu ya daraja hili wanatumia watembea kwa miguu. Ujenzi wa daraja hili umefikia katika hatua nzuri na kazi yangu ni kukusogeza karibu na matukio.

Leo May 4, 2017 wacha nikusogezee karibu na daraja la Furahisha jijini Mwanza kwa kukuwekea picha 8 za muonekano wa daraja hili.

KWA MSAADA WA MILLARD AYO

0 comments:

MWAKYEMBE AWAASA WAANDISHI WA HABARI

WAANDISHI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI

1-2
Na Nuru Juma & Husna Saidi- MAELEZO
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za uandishi katika kuandika habari zitakazoleta umoja,mshikamano na maendeleo na siyo uchochezi ili kujenga jamii bora.

Hayo yamesemwa leo  Jijini Mwanza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison George Mwakyembe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Dkt. Mwakyembe aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo siku hiyo huwa maalum kwa wadau wa tasnia hiyo kukutana na kujadiliana mambo mbalimbali  ikiwa ni njia ya kujenga jukwaa la ushirikiano.

“Uhuru wa habari una ukomo wake hivyo ni muhimu kwa   vyombo vya habari hapa nchini  kuajiri watu wenye taaluma hiyo kwa kuachana na makanjanja ili viheshimike kwa kutoa taarifa zenye kuzingatia maadili ya uandishi”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Alizidi kufafanua  kuwa katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kalamu ya mwandishi wa habari itetee ukweli na si mambo ya haramu kwa sababu ya siasa au rushwa ambayo huwa kichocheo cha uvunjifu wa amani.

Aidha aliitaka Idara ya Habari (MAELEZO) kuwa  na utaratibu wa kukutana na wahariri kila mwezi ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia nzima ya habari nchini.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi alisema uandishi wa habari si biashara ya kawaida bali ni kazi yenye kuhitaji uweledi mkubwa hivyo waandishi wanatakiwa kufuata taratibu na sheria za uandishi.

0 comments:

“Mimi na Dr. Slaa hatukusaliti vyama vyetu, tulisimamia misingi yetu” – Prof. Lipumba


Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa wasaliti ni waliomleta Lowassa ndani ya UKAWA na sio yeye na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Dr. Slaa kwa sababu walikuwa walisimamia misingi ya vyama vyao kama inavyosemwa.
Akizungumza kupitia Clouds 360 ya Clouds TV May 4, 2017, Prof. Lipumba amesisitiza kuwa aliwahi kumwambia Dr. Slaa kuwa anataka kugombea urais kupitia UKAWA, lakini naye Dr. Slaa alikuwa na nia hiyo.
“Mimi na Dr. Slaa hatukusaliti vyama vyetu, tulisimamia misingi yetu halisi ya vyama. Waliotusaliti ni wale waliomleta Edward Lowassa ndani ya UKAWA. Siyo sisi ambao tulijitoa ndani ya vyama vyetu.
“Nilizungumza na Dr. Slaa kuwa nilikuwa nataka kugombea Urais kupitia UKAWA-CUF, Dr. Slaa pia alihitaji kugombea.” Prof. Lipumba.

0 comments: