HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBER 1,

Magazetini ni leo Jumatano November 1, 2017



























0 comments:

News Alert : NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA - JKT 2017 ZATANGAZWA


TAARIFA KWA UMMA
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo anawatangazia vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2017.

Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa mikoa na wilaya ambapo muombaji anaishi.
Zoezi la kuchagua vijana litaanza Mwezi Novemba 2017 na vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 mpaka 09 Desemba 2017.
Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT haziuzwi, aidha yeyote atakaye husika na utapeli wa kuuza au kununua nafasi hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Sifa za mwombaji ni kama ifuatavyo:
  1. Awe raia wa Tanzania.
  1. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la Saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18.
  1. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne ni kuanzia miaka 18 hadi 20.
  1. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Sita ni kuanzia miaka 20 hadi 22.
  1. Vijana wenye elimu ya Stashahada na Shahada ni kuanzia miaka 23 hadi 25.
  1. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamili ni kuanzia miaka 26 hadi 27.
  1. Vijana wenye elimu ya Shahada ya Uzamivu ni kuanzia miaka 28 hadi 35.
  1. Awe na afya njema, akili timamu na asiwe na alama yeyote ya michoro mwilini (Tattoo).
  1. Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
  1. Kwa vijana waliomaliza elimu ya sekondari kidato cha nne, wawe waliomaliza kuanzia mwaka 2015, 2016 na 2017 wenye ufaulu wa alama (Points) zisizopungua 32.
  1. Awe na cheti cha elimu ya msingi aliyehitimu Darasa la Saba.
  1. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
  1. Awe na cheti halisi cha kumaliza shule (School Leaving Certificate).
  1. Awe na cheti halisi cha matokeo (Original Academic Certificate) na kwa wale waliomaliza shule mwaka 2017 wawe na Transcript au Statement of Result.
  1. Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au KMKM wala kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.
  1. Asiwe amepitia mafunzo ya JKT Operesheni za nyuma.
  1. Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo.
Aidha, Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa na pia kuwa na vifaa vifuatavyo:
  1. Bukta ya rangi ya Dark blue yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu. Aidha bukta za wanawake zinatakiwa kuwa na lastic magotini.
  1. Raba za michezo zenye rangi ya kijani.
  1. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  1. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
 Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,Makao Makuu ya JKT,
Tarehe 30 Oct 2017.

0 comments:

RC GEITA KUWAPIMA MAOFISA UGANI UWEZO WA UTENDAJI KAZI ZAO ZA KILIMO


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akimkabidhi mbegu bora ya mahindi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu za mahindi, mhogo na viazi lishe uliofanyika nje ya viwanja vya ofisi ya mkoa huo jana. Kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa mbegu hizo za mahindi zinazokabiliana na ukame Wema.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Isamilo kabla ya uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kutoka kushoto ni Mtafiti kutoka COSTECH, Dk.Beatrice Lyimo, Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, Mtafiti Bestina Daniel na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu ya mahindi.
Wananchi wa Kijiji cha Isamilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkulima Hernick Elias wa Kijiji cha Isamilo akizungumzia changamoto za kilimo walizonazo
Watafiti wakifanya vipimo kabla ya uzinduzi wa shamba la mbegu za mahindi katika kijiji cha Isamilo.
Wakulima wa Kikundi cha Nguvumoja cha Kijiji cha Isamilo wakiwa shambani wakati wa uzinduzi huo.
Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Salome Renatus akizungumza na waandishi wa habari.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla ya upandaji wa mbegu za mahindi.
Ofisa Ugani wa Kijiji cha Isamilo, Issa Pegeege, akionesha jinsi ya uwekaji mbolea kabla ya kupanda mbegu ya mahindi Wema.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari (kulia), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akiongoza wakulima kupanda mbegu ya mahindi kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Isamilo.
Mkulima wa Kijiji cha Kikundi cha Nguvu moja katika Kijiji cha Kamhanga, Hamisi King akitoa maelekezo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mahindi katika kijiji hicho.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla ya upandaji wa mbegu za mahindi katika Kijiji cha Isamilo. 
Wakulima na wananchi wa Kikundi cha Kasimpya katika Kijiji cha Mnekezi kilichopo Kata ya Kaseme wakisubiri maelekezo namna ya kupanda mbegu za mahindi katika shamba darasa.
Diwani wa Kata ya Kaseme, Andrew Kalamla akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shamba darasa hilo
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnekezi.
Mwakilishi wa Mkoa wa Geita, Emiri Kasagala, akihutubia katika uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, Robert Gabriel
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akipanda mbegu wakati wa uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Mnekezi. Kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Emiri Kasagala.Picha na Dotto Mwaibale, Geita
**
MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi amesema ataanzisha utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wa mkoa huo utendaji kazi wao ili kujua uwezo wa kila mmoja wao.
Hayo ameyasema wakati Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ilipokuwa ikimkabidhi mbegu bora za mahindi, mihogo na viazi lishe ikiwa ni siku yake ya kwanza kufanya kazi katika mkoa huo tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kushika wadhifa huo.
"Kilimo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo nitaweka utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wote wa mkoa huu ili niweze kujua utendaji kazi wao" alisema Lughumbi.
Lughumbi aliwataka maofisa ugani mkoani humo kuacha kukaa maofisi kwenye viyoyozi badala yake waende walipo wakulima kushirikiana nao kuwapa elimu ya kilimo ili kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo.
Mkuu huyo wa mkoa ameahidi kununua viatu vya shambani 'gambuti' na koti na kuwa mara moja ataanza kutembelea wakulima katika maeneo yao ili kujua changamoto zao na kusema anapenda kuona mkoa wa Geita unakuwa namba moja kwa kilimo hapa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa.
Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato na ukame.
Akizungumzia mbegu bora ya viazi lishe alisema mbegu hiyo viazi vyake vinavitamini A ya kutosha ambayo ni muhimu kwa watoto na hiyo itawasaidia baadhi yao kuto kwenda Hospitali kuipata badala yake wataipata kwa kula viazi hivyo.
Msangi aliwaomba maofisa ugani pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali za kazi yao wasisite kwenda COSTECH ili kusaidiana na kupeana mbinu mbalimbali za kilimo.
Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Hermick Elias alisema kukosekana kwa mbegu bora, wataalamu wa kilimo na kutofikiwa na pembejeo za kilimo kwa wakati ni moja ya sababu ambayo imewarudisha nyuma katika masuala ya kilimo lakini wanaamini kwa mbegu hizo walizoletewa na COSTECH itakuwa nu mkombozi kwao kwa kupata chakula na ziada watauza na kujipatia fedha za kuwasaidia.

0 comments:

UPDATES: Kinachoendelea Polisi Baada ya Zitto Kabwe Kukamatwa


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi.
 
Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo:
 
1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.
 
2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
 
Timu ya mawakili wa chama iko na ndugu Zitto katika mahojiano haya.
 
Ado Shaibu - Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi
ACT Wazalendo
Oktoba 31, 2017
Dar es salaam


0 comments:

Uhuru Kenyatta Atangazwa Mshindi Wa Urais Nchini Kenya Kwa Asilimia 98


Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha urais baada ya kujikingia kura 7,483, 895 sawa na asilimia 98 katika uchaguzi wa marudio uliosusiwa na mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.
 
Kwa matokeo hayo, Rais Kenyatta na makamu wake William Ruto walikabidhiwa vyeti vya ushindi na sasa Uhuru anasubiri kuapishwa kuiongoza nchi kwa miaka mitano ikiwa matokeo hayo hayatapingwa na kufutwa.
 
Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alitangaza matokeo hayo bila kura kutoka majimbo 25 ya eneo la Nyanza ambalo wafuasi wa Odinga walifanya vurugu na kusababisha uchaguzi kuahirishwa.
 
Chebukati alisema mazingira yaliyokuwa yameandaliwa kwa ajili ya uchaguzi wa marudio yaliwezesha kuwa wa kuaminika, huru na wa haki.
 
Akizungumza mapema, Makamu mwenyekiti wa IEBC Consolata Nkatha alisema kura za maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi hayawezi kuathiri matokeo ya mwisho.

Nkatha alisema mchakato ulikamilika katika majimbo 266 ambako uchaguzi ulifanyika na kwamba tume, kwa kuzingatia kifungu cha 55(B)(3) cha Sheria ya Uchaguzi ambacho kilielekeza marudio kufanyika na hivyo kusafisha njia kwa rais mteule kutangazwa.
 
Alhamisi iliyopita, ulifanyika uchaguzi mpya wa marudio kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Juu katika uamuzi wa jumla Septemba Mosi uliobatilisha ushindi wa Rais Kenyatta wa Agosti 8 kwa madai ya kuwepo kasoro na dosari zilizofanywa na IEBC.
 
Odinga alisusia uchaguzi wa marudio akitaka, pamoja na mambo mengine wafukuzwe maofisa wa tume na mchapishaji wa makaratasi ya kura na msambazaji wa vifaa vya kiteknolojia.
 
Hata hivyo, ilikuwa vigumu kuandaa uchaguzi katika majimbo 25 Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori ambako Odinga anaungwa mkono.
 
Katika majimbo mengi, uhuni ulikithiri kiasi cha kuzuia kabisa upigaji kura wa marudio kwani walifunga mageti na kuchomelea kwa nondo na wengine walizusha ghasia kiasi kwamba IEBC ilishindwa kuwalinda maofisa wake.
 
Chebukati alisema Ijumaa iliyopita kwamba maofisa wa uchaguzi walitishwa, walitekwa au kuteswa na akasema ilitilia maanani sana kokote ambako maofisa wake walikabiliwa na vitisho.

Uchaguzi ulifanyika katika majimbo 265 kati ya 290 ya Kenya yakiwemo ya nje ya nchi ambapo Wakenya waishio Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika walipiga kura.
 
Katika majimbo 266 Rais Kenyatta alipata kura 7,483, 895 yaani kura 719,395 chini yakura 8,203, 290 alizopata katika uchaguzi uliofutwa.
 
Kwa kura 7,616, 21 halali zilizopigwa katika majimbo 266 yaliyoshiriki uchaguzi, idadi hiyo ni sawa na asilimia 42.36 wakati ikipigiwa hesabu kwa watu 19, 611, 423 waliojiandikisha walioshiriki uchaguzi wa Alhamisi walikuwa asilimia 38.84.
 
Uchaguzi wa Agosti 8 waliojitokeza walikuwa asilimia 79.17 idadui ambayo ilikuwa pungufu ikilinganishwa na mwaka 2013 waliposhiriki asilimia 86 ambao Kenyatta alimshinda Odinga katika kinyang’anyiro kikali. Odinga alipinga matokeo lakini alishindwa Mahakama ya Juu.

0 comments:

Wizara Ya Afya Yatoa Tahadhari Ya Ugonjwa Wa Marburg


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), mnamo tarehe 19 Oktoba 2017 kuhusu ugonjwa wa Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda tangu tarehe 17 Octoba, 2017. Maeneo yaliyoathirika  na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kween, Kanda ya Mashariki ya nchi, ambayo  inapakana n nchi ya  Kenya. Hadi kufikia  tarehe 19 Oktoba 2017, watu 4 walikwishapata maambukizo ya ugonjwa huo, ambapo wawili kati yao   wamepoteza maisha.

Wizara  inatoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi  katika mikoa yote ya Tanzania, hususan kwa wale wanaoishi  katika mikoa ambayo inapakana na na nchi  ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera).

Ugonjwa wa Marburg  unafanana sana na ugonjwa wa Ebola. Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg vinajulikana kama  “Marburg Virus”, navyo vipo katika jamii moja na virusi vinavyosababisha Ebola (Ebola virus). Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinazosababisha kutokwa damu mwilini, (Viral Haemorrhagic Fevers). Ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo.

Dalili kuu za ugonjwa huu ambazo huanza ghafla ni pamoja na Homa kali, maumivu makali ya kichwa pamoja na mwili kuishiwa nguvu ambapo baadaye huambatana na kuharisha sana (majimaji), maumivu ya tumbo, kichefuchefu na kutapika na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili yaani pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, masikioni, machoni, hali inayopelekea kifo kwa muda mfupi. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 3 hadi 9 baada ya kupata maambukizi.

Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na ha­raka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine iwapo mtu atakuwa karibu na mgonjwa na kugusana na mate, damu, mkojo, machozi, kamasi, maji maji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na jasho au kumgusa  mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Marburg. Ugonjwa huu pia unaweza kuenezwa iwapo mtu atagusa nguo au mashuka ya mgonjwa wa Marburg.

Wizara ya Afya , imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:

Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kupitia OR-TAMISEMI. Taarifa hiyo imejumuisha namna  Ukweli kuhusu ugonjwa (Fact sheet),

Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya na maeneo ya mipaka ya nchi kavu na maji. Aidha watalaamu hawa wa Afya pia wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu ili endapo ugonjwa huo utatokea uweze kutolewa taarifa mapema na kushughulikiwa.

Vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya na vipima joto maalum (thermoscan) tayari vipo katika maeneo husika ya mikoa.

Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani hadi  sasa hakuna mgonjwa yeyote wa Marburg aliyeripotiwa nchini. Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo cha huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huu.

Kitengo cha mawasiliano ya Serikali

30/10/2017

0 comments:

Serikali yamjibu Zitto Kabwe......Yampa ONYO Kali

Na.Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni.

Taarifa hizo za Mh. Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.

Onyo hilo limetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Bw. Daniel Masolwa Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS),kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS,pamoja na  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Johnson Nyella wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari.

Masolwa alisema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na Mh. Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa juhudi znazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano hazina manufaa kwa Wananchi.

“Napenda kukanusha kauli ya Mh. Zitto kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za Pato la Taifa zimepikwa, Mh. Zitto anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za Pato la Taifa ni ya kitaalam na inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu na Shirika la Fedha Duniani (IMF)”,alisema Masolwa.

Aliongeza kuwa miongozo hiyo ni pamoja na mifumo ya pato la Taifa ya mwaka 2003 na 2008 na mwongozo wa kuainisha shughuli za kiuchumi Toleo la Nne ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka  2016 Tanzania imekuwa nchi ya pili kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kwa utoaji, uchambuzi, usimamizi na usambazaji wa takwimu  kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Aidha Bw.Masolwa alitoa wito kwa taasisi yoyote ile au mtu binafsi anayetaka kutayarisha takwimu rasmi  kwa ajili ya kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo kupata maelezo ya kina kuhusu ukokotoaji na miongozo mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella alisema kuwa Mh. Zitto amekokotoa ukuaji wa Pato la Taifa anaodai kuwa ni sahihi kwa kuangalia tofauti kati ya ongezeko la ujazi wa fedha na mfumuko wa bei jambo ambalo sio sahihi kulitumia kama kipimo.

“Ukokotoaji wa aina hiyo umejengwa juu ya nadharia inayoitwa ‘quantity theory of money’ ambayo inasema mfumuko wa bei hutokea pale fedha zinapoongezeka kwa kasi zaidi kuliko uzalishaji wa vitu halisi ambayo si sahihi kutumia nadharia hiyo kuelezea mfumuko wa bei na ukuaji wa uchumi katika kipindi cha muda mfupi kama Mh. Zitto alivyofanya,” alifafanua Bw.Nyella.

Wawakilishi hao wa Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wamelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa za Ukuaji wa Pato la taifa kutolewa na Mh.Zito, na wakawaasa Wananchi na wanasiasa kuacha kupotosha takwimu za serikali na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kupotosha umma kwa makusudi.

0 comments:

ZITTO KABWE MIKONONI MWA POLISI

TAARIFA KWA UMMA

ZITTO KABWE AKAMATWA

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo,Zitto Kabwe,amekamatwa na jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake na anapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe

Sababu za kukamatwa kwake ni hotuba ya juzi katika kata ya Kijichi

Abdallah Khamis

Afisa Habari
ACT Wazalendo
0655549154

0 comments:

ALICHO KISEMA JOSEPH YONA JUU YA RAZALO NYALANDU

CCM MPYA NA TANZANIA MPYA AKINA LAZARO NYALANDU HAWATAKIWI.

Na Joseph Yona

     

Kwanza kabisa nianze kumshukuru kipenzi chetu Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Joseph John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazo zifanaya hasa kurudisha Tanzania yetu ambayo ilikuwa imepotea katika ramani ya haki na maendeleo.

Napenda niseme kwamba Dr Magufuli akili nyingi bana,na kwa moyo mkunjufu niseme tu hongera Rais wetu kwa uzalendo huo unaotuonyesha watanzania muda wote yeye anafikiri juu ya watanzania na Tanzania, na ndio maaana alikuwa  halidhishwi na uongozi wa wizara ya utalii zamani wa Prof  Jumanne Magembe, aliamua kumuondoa na kumuweka mchapakazi Dr Hamis Kigwangala

Dr Kigwangala katika  wizara hii  ni kama shamba la bibi,kaamaua kwa muda mchache kupiga kazi na leo tarehe 30 october 2017 kimetokea kile kilicho kuwa kimetarajiwa   kwani aliye kuwa waziri wa wizara hiyo mzee wa matumizi na starehe Razalo Nyalandu ameondoka CCM

Kwangu mimi kuondoka kwa Razalo Nyalandu nilitegemea,siku itokee kwa kuwa anayo makando kando mengi ambayo tukiamua kuyasema anatakiwa akamatwe na afungwe maisha.

Leo tunapigania ccm mpya na Tanzania Mpya, nchi na chama cha Rais na mwenyekiti aliye na halufu nzuri katika uongozi na uzalendo wa kweli,watu kama Razalo Nyalandu watupishe walejee kwenye chama chao cha mafisadi kama CHADEMA.

Nani asiyejua kuwa Kuna kipindi Mbunge wa arumeru Joshua Nasari aliwahi kuongea kwa uchungu sana Namnukuu :-
Mh. Spika dalili za serikali iliyochoka ni Kama ya kuwa na Mawaziri Kama Razalo Nyalandu.
Anaendelea Yaani waziri wa maliasili kazi yake ni:-
Kupiga Picha na Mbwa wa wazungu,kupiga Picha ameshika risasi,kupiga Picha na helcopiter,kwenda na mamiss Kama Kina Anti Ezekiel nje ya nchi,tena kazi yake kubwa ni Kupiga Picha amebeba askari wa kike wa wanyamapori akiwa amemshika makalio na kumshika bega.
Mwisho Nassari aliomba uwaziri wa mambo ya ndani kumfundisha na kuwafundisha adabu sasa leo amepatikana Rais makini anayetaka maliasili zetu ziwanufaishe Watanzania wote hakika Razalo Nyalandu hafai kubaki CCM MPYA

Pia Nyalandu atambua kuna kipindi mbunge wa iringa mjini waziri kivuli wa maliasili aliwahi kumtuhumu kuwa ameuza nyala za serikali na kuruhusu zisafirishwe nchi za nje na biashara ya meno ya tembo ilishamili nchini chini ya uongozi wake Nyalandu.

Na hata biashara za ujangili pamoja na biashara  haramu ndani ya mbuga zetu za Taifa  zilisikika kila kona ya dunia na yeye akiwa kama kiongozi mwenye dhamana waziri wa wizara ya Maliasili na Utalii.

Leo Nyalandu bila hata kumuogopa Mungu anatamka CCM hii imepoteza uwelekeo,ila kipindi kile anakula bata kwenye shangingi la Waziri huku akitafuna chops za ngiri wa mikumi na ma miss wetu aliona ccm inafaa na iko katika uelekeo sahihi.
Wakati anashutumiwa kutafuna billion mbili za maliasili hapo ccm ilikuwa sawa chaaa!!!!

Wakati waziri huyo kivuli anakushutumu akionyesha video inayobainisha namna baadhi ya kampuni za uwindaji nchini zinavyo tumia vibaya leseni zao hapo ccm ilikuwa sawa aisee!!

Pia haya yote yanatokea kuna jangili kadakwa huko mbugani akiwa na risasi mia tatu hamsini na nane (358),nasikia amebanwa ataje mabosi zake na hii inanifanya nirudishe kumbukumbu kwenye Vita takatifu ya madawa ya kulevya aliyowahi piganiwa Paul Makonda,sasa Dr Kigwangala ameingia katika vita takatifu nyingine  watanzania tumuunge mkono kwa kutoa ushirikiano.

Lakini vile vile nyalandu asitufanye tulio lala tukaamka,Nyalandu nakumbuka mkataba mbovu alioingia na wamarekani katika Mbuga yetu muhimu ya Selous wa kuchimba madini ya urenium,na anajua rais alivyo mkali kwenye Madini.

Nyalandu hajui kuwa alikuwa anataka kuwamilikisha wamarekani umiliki wa loliondo wa miaka mingi zaidi sema usalama wa taifa walikataa na akashindwa jaribio hilo.

Nyalandu hajui kuwa tunajua kuwa alimruhusu mkewe Faraja Kota kuuza vitaru  vya wanyama poli kiholela ndani ya mbuga ya selous.

Nyalandu hajui kama tunajua maisha yake ya uwaziri alikuwa akanyagi ofisini au wizarani,ila kazi za wizara alikuwa akizifanyia hotelini southern sun.Yaani hajui tulikuwa tunapishana na mafaili ya wizara korido ya southern sun na kutumia gharama nyingi za wizara kufanyia kazi za wizara hapo hotelini kula kunywa na nk.

Au Nyalandu hajui kuwa tunajua alitumia mabilioni kwa mabilioni eti kutangaza mlima kilimanjaro ndani ya uwanja wa sunderland kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Au hajui  kuwa mgogoro mkubwa na bodi ya utalii TTB  walikwazana nae mwanzo,kabla hajawakamata kwa hongo bodi ilimshauri aangalie taratibu za manunuzi vizuri zisikiukwe akakataa na akaiingiza wizara hasarani naamini mpaka Leo wanalipa.

Pia hajui kuwa tunajua aliye kuwa mwiba mgumu kwake ni aliye kuwa mkurugenzi wa TTB  Dr.Nzuki aliye mlazimisha akakataa,akawakamata wajumbe wa bodi hiyo akawashawishi wa muondoe Dr Nzuki kwa vyombo vya habari.

Au haju alivyo muondoa Dr.Nzuki akampeleka chuo cha utaliii na Dr Nzuki akaondoka kwenda Dubai.

Au Nyalandu hajui kuwa sisi masikini tuna mfuatilia sana Rais wetu mpendwa Dr Magufuli kuwa baada ya kuingia tu madarakani alichukua uwamuzi wa kumrudisha Dr.Nzuki na kumpa nafasi ya kuwa Naibu katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na utalii.

Mwisho wenzangu na sisi ambao tunaona muelekeo mpya kabisa wa uzalendo anao chukua Rais wetu Dr Magufuli tunaendelea kumuunga mkono Rais kwamba yuko njia sahihi. Dr kigwangala upo njia sahihi songa  fumua na weka mambo sawa ili watanzania wafaidi.

mwandishi ni

 Mwenyekiti wa ccm tawi la bokorani na managing director wa pavea blog.
JOSEPH YONA.
0713 802 226.
0622 222 787.

0 comments: