VIJIJI 126 VYAPATIA MRADI WA UMEME MKOANI SHINYANGA
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida.
WANAKIJIJI
wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi
wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani
Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi.Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.
Bi Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo, Desemba 22, 2016.
“Nia ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa mwananchi
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya kuunganishiwa
umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la
thamani VAT.” Alisema.
Alisema, kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la Umeme, TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa Wakala wa Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi huu wa Backbone kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu ya umeme na kwa bei nafuu.” Aliongeza.
Alisema, Serikali kupitia TANESCO imepiga hatua kubwa ya kuwafikishia umeme wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya wananchi wa Tanzania wamepatiwa huduma ya umeme.
Akizungumzia kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara na njia za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa kuwasha kipande kilichokuwa hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.
Mradi huo ulianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2013 na unafadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo umegharimu karibu shilingi Trilioni 1.
Kazi iliyokuwa ikifanywa ni pamoja na ujenzi wa minara mikubwa yenye uwezo wa kubeba nyaya 6, tatu kila upande tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kubeba nyaya 2 tu moja kila upande. “Lakini pia kazi nyingine iliyokuwa ikifanyika chini ya mradi huu, ni upanuzi wa vituo vinne vya kupoza na kusambaza umeme, vituo hivyo ni kile cha Iringa, Zuzu, mkoani Dodoma, Kibaoni mkoani Singida, na Ibadakuli mkoani Shinyanga Shinyanga.” Alifafanua
0 comments: