Emily Adolph:Miss Tanzania Aliyezua Gumzo Kubwa 1995!

Huyu Ndiye Miss Tanzania Aliyezua Gumzo Kubwa 1995!



Kushinda lile la Sitti Mtemvu mwaka juzi! ( Kutoka Maktaba ya Mwenyekiti, Majid Mjengwa.

Ilikuwa Septemba 3, 1995, Daily News liliripoti, kuwa msichana wa miaka 18, Emily Adolph, pichani, Mwanafunzi wa Central Secondary School, Dodoma, ndiye Miss Tanzania.

Hakukuwa na social media wakati huo, lakini mjadala wa kwenye jamii ulioibuka. Ule wa Sitti Mtemvu mwaka juzi hauwezi kuufikia. Tuliokuwepo tutakumbuka, kuwa tuliuona ni mjadala wa ajabu kuwahi kutokea, maana mambo ya U-Miss nayo yalikuwa mapya kwetu.

Ikafika mahali mpaka Serikali ikaingilia kati kwa kumtafutia shule Emily baada ya kufukuzwa shuleni kwake..!
Tatizo lilikuwa umri wake, kuwa ulikuwa ni mdogo, wakati Sitti Mtevu tatizo lilikuwa hilo hilo la umri, alituhumiwa kufoji umri!
Sijui Emily Adolph yuko wapi sasa?
Kwa msaada wa Maggid Mjengwa,
Iringa.

0 comments:

BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM WILAYA YA KUSINI UNGUJA MAREHEMU HAMDANI



index
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MJUMBE wa Kamati kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Idd ameongoza mamia ya wanachama wa Chama na Wananchi kwa ujumla katika mazishi ya  aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja Marehemu Hamdani Haji Machano aliyefariki ghafla jana kwa maradhi ya baridi.

Maziko hayo yamefanyika  katika kijiji cha Donge Shehia ya Mtambile Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kuudhuriwa na wananchi  pamoja na baadhi ya  wajumbe wa kamati kuu, Halmashauri kuu za CCM, Wenyeviti , Makatibu wa Mikoa na Wilaya,  Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Zanzibar pamoja na Wajumbe wa NEC.

Akizungumza mara baada ya maziko hayo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dkt.Abdalla Juma Saadalla “Mabodi ”  alisema Chama hicho kimepokea kwa mshituko na masikitiko  makubwa taarifa ya kifo cha Mtendaji huyo na kuwaomba wanafamilia, ndugu na jamaa kuwa na subira katika kipindi hiki cha msiba.

Ameeleza kwamba marehemu Hamdani alikuwa ni  Kiongozi mwadilifu na mchapakazi na aliyekuwa akijitolea kufanya kazi kwa bidii huku akisimamia kwa dhati maslahi ya Chama hicho.
Dkt.Mabodi alifafanua kwamba kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na marehemu huyo wakati wa Utumishi wake, CCM itaendelea kuenzi juhudi hizo kwa kusimamia mamlaka za kiutendaji ndani ya chama na serikali ili ziendelee kutenda haki kwa wananchi wote.

“Tumepokea kwa mshituko mkubwa kifo cha Mtendaji mwenzetu na hili ni pengo kubwa linalotakiwa kuzibwa na umoja wetu katika na kukitumikia chama chetu kwa uzalendo ili kishinde kila uchaguzi na kuendelea kuongoza dola kusimamia yote mazuri yaliyoachwa na Marehemu Hamdani.

Pia nakumbuka hivi juzi tu katika ziara zangu tulikuwa pamoka katika Mkoa wake wa kazi tukishauriana mambo mengi ya Kiutendaji na kisiasa, naomba Mwenyezi Mungu amjaalie mapumziko mema na yenye kheri na yeye Amin.”, alieleza Dkt.Shein.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka aliweka bayana kwamba Marehemu Hamdani alisema kwamba ni kada wa kweli yaliyepigana kuona  CCM na Jumuiya zake zinapiga hatua kubwa kimaendeleo.

Naye Mkaazi wa Shehi ya Chanjaani, Masoud Haji Choum alisema mbali na Marehemu huyo kuwa na ushirikiano mzuri na viongozi wa chama na serikali pia alikuwa ni mtu aliyekuwa akipenda kujumuika na jamii katika masuala mbali mbali ya kimaendeleo, kijamii na kiuchumi.

Akithibitisha mchango wake Marehemu huyo katika harakati za kisiasa ndani na nje ya Naibu Katibu Mkuu Mstaafu, Vuai Ali Vuai Alieleza kwamba Hamdani alikuwa ni mtu makini na mkweli katika utumishi wake na aliyetamani mabadiliko ya kimaendeleo katika sehemu yake ya kazi na chama kwa ujumla.

Mara baada ya maziko hayo palisomwa wasifu wa marehemu Hamdani kuwa alizaliwa mwaka 1963, huko Donge.
Amewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi na utendaji ndani ya chama na jumuiya zake baada ya kujiunga na CCM mwaka 1987 ambapo mwaka 1988 alikuwa katibu wa UVCCM Tawi la Donge Mtambile mwaka, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kusini hadi kufikiwa na mauti alikuwa ni Katibu wa CCM Wilaya ya  Kusini Unguja.

Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Amin.

0 comments:

MAJALIWA:MABALOZI WA TANZANIA TANGAZENI VIVUTIO VYA UWEKEZAJI NA UTALII


KASSIM-MAJALIWA
Waziri mkuu Kassim Moajaliwa amekutana na mabalozi wa Tanzania wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanaimarisha uhusiano na kujenga urafiki kati ya nchi  wanazowakilisha kwa lengo la kuitangaza Tanzania kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kueleza fursa za uwekezaji na utalii  zilizopo nchini.

Mabalozi wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,kuwakilisha  Tanzania nnje ya Nchi,wamefika ofisi ya waziri mkuu mjini Dodoma kwa lengo la kumuaga na kwenda kuanza majumukumu yao katika nchi walizopangiwa.
Waziri mkuu amewaleeza mabalozi hao kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji Na jukumu lao  la kwanza la  Mabalozi hao  ni kuvitangaza vivutio vilivyopo ili kuleta wawekezaji wengi TANZANIA .

Suala la ushirikishwaji sekta binafsi pia waziri mkuu amesema Tanzania imelipa kipaumbele
Waziri Mkuu alizungumzia sula la watanzania waishio nje ya nchi , aliwataka Mabalozi kuwakutanisha na kufanya nao mikutano mara kwa mara ilikujua kama wanamatatizo yanayoyapata katika nchi wanazoishi ilikuangalia jinsi gani wanaweza kusaidiwa,

Mabalozi hawa wanaenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi za QATAR,UBELIGIJI,AFRIKA KUSINI,UJERUMANI,COMORO,ALGERIA,INDIA NA ,SUDAN.

0 comments:

MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA SEKONDARI YA CHANG’OMBE MAZOEZI YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM


P 1
Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang’ombe Mazoezi, Daina Matemu, akimuongoza kuelekea kwenye ukumbi wa mahafali, mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya shule hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (kushoto), wakati wa mahafali hayo, yaliofanyika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE). Nyuma kulia ni Mwenyekiti Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)  

Kijana wa Skauti kutoka shule hiyo, akimvisha skafu Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha, mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mahafali hayo. Anayeangalia ni Mkuu wa shule hiyo, Daina Matemu. 

Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (wa pili kulia), akiwa na wageni mbalimbali kwenye meza kuu wakipiga makofi mara baada ya kuasili ukumbini.

Wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Chang’ombe Mazoezi, wakiimba wimbo wa shule hiyo, mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha, wakati wa mahafali yao leo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang’ombe Mazoezi, Daina Matemu, akizungumza wakati akitambulisha wageni mbalimbali kwenye meza kuu katika mahafali hayo.

Mgeni rasmi akiwa na wageni mbalimbali kwenye meza kuu wakimwombea mmoja wa wanafunzi aliyefariki wakati wakiwa kidato cha tano, wahitimu hayo. 

Wahitimu wa kidato cha sita wakimwombea mwenzao aliyefariki wakiwa kidato cha tano.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang’ombe Mazoezi, Hussein Chiumbi, akisoma taarifa ya shule hiyo katika mahafali hayo. 

Baadhi ya wahitimu wakicheza ngoma za Bongo Fleva, wakati walipokuwa wakionesha vipaji vyao.  

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma, Elly Mdundo, akitoa taarifa ya maendeleo ya taaluma kwa mgeni rasmi. 

Baadhi ya walimu wa shule hiyo, wakiwa katika mahafali hayo. 

Mhitimu wa kidato cha sita, Mansoor Mohamed akisoma risala ya wahitimu. Anayemsaidia ni mhitimu mwenzake, Hefsiba Nyangi.

Wahitimu wa kidato cha sita, Mansoor Mohamed na Hefsiba Nyangi wakimkabidhi risala ya wahitimu mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha.

Baadhi ya wazazi, ndugu na jamaa za wahitimu wa kidato cha sita, wakiwa katika mahafali hayo. 

Baadhi ya wahitimu wakionesha mitindo ya mavazi yaliyobuniwa na shule hiyo. 

Baadhi ya wahitimu wakipita na mavazi yaliyobuniwa na shule hiyo. 

Baadhi ya wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha na mavazi yaliyobuniwa na shule hiyo. 

Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang’ombe Mazoezi, Daina Matemu, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta (kushoto), ili amkaribishe mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (katikati), azungumze na wahitimu hao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta, akizungumza katika mahafali hayo, wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (katikati), azungumze na wahitimu hao. 

Mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Chang’mbe Mazoezi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha, akizungumza na wahitimu wakati wa mahafali hayo, yaliofanyika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), jijini leo. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta na kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Daina Matemu.

0 comments:

MAHAFALI YA PILI YA KIDATO CHA SITA WAMA NAKAYAMA YAFANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wanafunzi kote nchini kupenda kusoma masomo ya Sayansi hasa watoto wa kike ili Taifa liweze kujitosheleza kwa wataalamu wa fani mbalimbali nchini hasa wakati huu ambao Taifa linaelekea kwenye uchumi wa Viwanda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya sekondari ya WAMA- NAKANYAMA Jijini Dar es Salaam, mahafali ambayo imehudhuriwa na wake wa Marais Wastaafu.

Makamu wa Rais amesema haitapendeza hata kidogo ajira nyingi nchini kuchukuliwa na wataalamu mbalimbali mataifa ya nje hasa kipindi hiki wakati Serikali inahimiza ujenzi wa viwanda hivyo amesisitiza wanafunzi wajikite kwenye kusoma masomo ya sayansi ili taifa liweze kujitosheleza kwa ajili ya manufaa ya maendeleo ya taifa. Amesema katika kuhakikisha taifa lipata wanasayansi wengi, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa maabara na kununua vifaa vya maabara ili kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kupenda kusoma masomo ya sayansi kote nchini.

Makamu wa Rais pia amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inakusudia kuimarisha ufundishaji wa masomo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano –TEHAMA- katika shule za Sekondari na kujenga maabara za kompyuta nia ikiwa ni kuongeza wataalamu wa fani hiyo nchini. Kuhusu mila na desturi kandamizi kwa wanawake na wasichana zilizopo kwenye baadhi ya jamii nchini, Makamu wa Rais ameitaka jamii kukomesha mila hizo na iwashirikishe wanawake katika mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi kwani watakuwa ni chachu ya maendeleo katika jamii husika.

“Wote tunajua wanawake ni chachu na kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii, Taifa na Dunia kwa ujumla hivyo ni wajibu wa jamii kushirikisha wanawake katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo kote nchini” amesisitiza Makamu wa Rais.



Makamu wa Rais pia ameipongeza Taasisi ya Wanawake na Maendeleo – WAMA- kwa kujenga shule Mbili za Sekondari na kusomesha watoto wanaotoka kwenye familia maskini na yatima na kusema huo ni mfano wa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo katika kusaidia kundi hilo ili watoto wanaotoka kwenye familia maskini nao waweze kuapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae. 


Kuhusu changamoto zinazoikabili shule ya WAMA – NAKAYAMA, Makamu wa Rais ameahidi kushughulikia changamoto hizo ikiwemo uhaba wa maji, ubovu wa barabara kuelekea kwenye shule hiyo na tatizo la uhaba wa mabweni.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama SALMA KIKWETE amesema aliamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo inamiliki shule Mbili mpaka sasa ili kusaidia watoto wa maskini na yatima kupata elimu bure ambapo mpaka sasa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaliohitimu katika shule hizo ambao wamejiunga na masomo ya elimu ya juu.

Mama Salma Kikwete ameshukuru ushirikiano mkubwa anaopata kutoka Serikalini unaolenga kuhakikisha shule zinazoendeshwa na taaisisi hiyo ikiwemo ya Wama – Nakayama zinafanya vizuri.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiangalia kwa vitendo majaribio ya kiyasansi kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya WAMA NAKAYAMA kwenye sherehe za mahafali yao ambapo wanafunzi 45 wamehitimu. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete(kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa WAMA Bi.Zakhia Meghji wakiimba wimbo maalumu wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ambapo wanafunzi 45 wamehitimu.
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari WAMA NAKAYAMA.

0 comments:

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wateule

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazunguzo na Mabalozi Wateule wanaoenda kuiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani.Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma, yalijikita katika kujadili namna bora ya kuiwakilisha Tanzania ughaibuni kwa kuzingatia sera ya nchi ya mambo ya nje, kwa lengo la kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo, na kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya nchi yetu ikiwemo kutangaza shughuli za utalii zinazopatikana nchini.


Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo 


Balozi Mteule Baraka H. Luvanda akichangia jambo wakati wa mazungumzo. Punde baada ya mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri, Mabalozi walikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Katibu Mkuu Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima akiongea na Mabalozi ofisini kwake mjini Dodoma

Mazunguzo yakiendelea

0 comments:

Prof. Kitila asaini kandarasi za zaidi ya bilioni 600 kupeleka maji Tabora na Shinyanga vijijini

https://swahilitimes.com/wp-content/uploads/2017/04/mkumbo.jpgKatibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesaini kandarasi zenye thamani ya dola za Marekani Milioni 268.35 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 600 za Tanzania mjini Tabora kwa mkopo wa benki ya Exim ya nchini India kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria na kupeleka katika Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Igunga, Uyui, Shinyanga Vijijini na Nzega. 

Utekelezaji wa mradi ni wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya Mradi ilikuwa kufanya usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi, kazi ambayo ilifanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India na ilikamilika mwezi Desemba 2015. 

Awamu ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India. Sehemu ya Pili inaanzia Mjini Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni ya Shriram zote kutoka India.
Sehemu ya tatu inaanzia Nzega mjini hadi Igunga mjini, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Afcons ikishirikiana na kampuni ya SMC zote kutoka India. Usimamizi wa mradi unafanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India.

Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo naVisay Uplenchwar wa Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd akisaini Mikataba ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka kijiji cha Solwa Shinyanga na kupeleka maji Nzega.Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akimsalimia waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Lwenge
 Waziri
wa maji na Umwagiliaji Eng. Gerson Lwenge akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa
Tabora wakati alipowasiri katika viwanja vya Furahisha Tabora.

0 comments:

RC MAKALLA APOKEA MSAADA WA MIFUKO 400 YA SARUJI KUTOKA AKIBA COMMERCIAL BANK

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Amos Makalla amepokea msaada wa mifuko 400 ya saruji,kutoka kwa Benki ya AKIBA Commercial Bank Ltd ,kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa njia za Wagonjwa,yenye urefu wa mita 175 katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza hayo jana jijini Mbeya wakati wa kupokea msaada huo,RC Makalla aliwashukuru Wadau hao kwa kujitolea na kulishughulikia ombi lake kwa haraka na kwa uzito wa juu kabisa.

"Nawashukuru sana Wadau AKIBA Commercial Bank Ltd , kwa kulishughulikia ombi langu hili, ambalo sikutarajia kama lingechukua muda mfupi hivi,nawashukuru sana na nawaomba msichoke na  tuendelee kuijenga Mbeya yetu kwa pamoja",alisema Makalla.

Makala alisema kuwa kupitia kwa marafiki wa hospitali ya Mkoa,wanaoishi ndani na nje ya mkoa huo,kupitia harambee walioifanya hivi karibuni wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa mita 55 na na kuwa awamu ya pili inaendelea kwa ujenzi wa mita 175.

Mh.Makalla alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi huo,zilitumika fedha jumla ya shilingi milioni 600,kutokana na mahitaji kuwa makubwa ya ujenzi,ujenzi  ukasimama. kwa sababu zilikuwa zikihitajika fedha nyingine kiasi cha shilingi milioni 55,ndipo wakachukua hatua za kuomba msaada zaidi kwa wadau ambao ni AKIBA Commercial Bank Ltd .

"Kukamilika kwa ujenzi huu kutaondoa tatizo la wagonjwa kupelekwa au kwenda wodini kwa taabu, kwani wakati wa mvua tatizo linakuwa kubwa ",alisema Mh Makalla.

Kwa upande wa Akiba Commercial Bank kupitia kwa Afisa Masoko na Uendeshaji Bi Dora Saria amesema waliguswa sana baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa kutokana na wananchi kupata shida hasa wagonjwa kwenda wodini au kupeleka maiti kwenye chumba cha kuhifadhia maiti

Hivyo wao kama taasisi ya Benki waliguswa na jambo hilo,na wakachukua hatua ya kuchangia shilingi milioni 5 sawa na Mifuko 400 ya saruji na kuahidi kutoa Mafunzo na mikopo kwa wajasiriamali
Aidha Akiba wamevutiwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa kuliweka jiji safi hivyo watatoa Vifaa vya usafi na kushiriki kufanya usafi mwisho wa mwezi huu.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Amos Makalla akikabidhiwa mifuko 400 ya saruji na Bi. Dora Saria ambaye ni Afisa Masoko wa Akiba Commercial Bank Jijini Mbeya.Na Mr.Pengo wa Globu ya jamii Mbeya

RC Makalla akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi na wafanyakazi wa Benki ya Akiba na Serikali kwa ujumla.

0 comments: